Monday, May 19, 2014

G NAKO ALIVAA SHATI LILILOTOBOKA KWENYE LAUNCH YA CLOUD9

Jamani duh, kama mlifika jana kwenye uzinduzi wa season Mpya ya clouds9 basi mtakuwa mliona sehemu ambayo G NAKO A-town finest alipopanda stejini na shati tobotobo yaani likiwa limetoboka either kwa kuliwa na panya au mbu wa Dengue.
Gnako ambae alikuwa anaimba gere kwa hisia kali za kuchana mzuka ulimpanda akavua shati akabaki na tshirt ndani ambayo ilikuwa na matundu mawili , moja kwenye mkono wa tshirt na juu kidogo ya kifua,
G nako ambae aliwapagawisha mashabiki wake na vibao murua alivyoimba kwa mbwembwe zote alishangiliwa kwa nguvu na alimalizia na kibao matata alichopiga bo bo bonge moja la chorus cha Mfalme cha Mwanafa.
kwa mbwembwe nyingi alifunga duru hilo huku akishangiliwa na mashabiki wake na kupiga nao piga huku akiwa amevua shati lake lililotoboka na kuweka begani.
mzee kauwa. gwarawara weusi ni mmoja kati ya wanamuziki wakali sana wa chorus na style yake matata.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.