Kufuatia Mzee mmoja kujitokeza na familia yake na kudai kuwa eti ametapeliwa kwa njia ya mtandao na msanii Mrisho Mpoto, yeye mwenyewe amejibu kuwa kwa siku tatu zilizopita ameibiwa page yake ya facebook yenye watu zaidi ya elfu 50, sasa aliyeiba page hiyo ndo anawatapeli watu kwa kujidai eti kuna mkopo unatolewa na taasisi ya Vicoba, na mpaka leo Mpoto hawezi kufanya lolote kwenye page hiyo, yani si yake tena, Hali hiyo imesababisha msanii kuahidi donge nono la milioni moja kwa mtu atakayewezesha kurudisha page hiyo.
Maharamia hao wamepost kwenye page ya www.facebook.com/mrishompoto
HABARI MUHIMU KWA WATANZANIA WOTE.
#BREAKING_NEWS:
Taasisi ya Vicoba Tanzania imezindua rasmi mtandao / tovuti http://focus-vicoba.wapka.mobi/
kupitia mfuko wa utoaji mikopo kwa watanzania wote uitwao FOCUS VICOBA
ili kurahisisha upatikanaji mikopo kwa haraka kwa watanzania na kumuwezesha
kila mtanzania kujiunga vicoba na kupatiwa mkopo popote pale alipo kwa
urahisi zaidi. Mtanzania ataweza kutembelea tovuti yao http://focus-vicoba.wapka.mobi/ na akajiunga kwa kujaza fomu zao na kuweka akiba zake na kupatiwa mkopo. Ni rahisi, salama na haraka.
Riba nafuu pia zawadi za bajaji na boda boda zinatolewa kwa watakao
chukua mkopo mkubwa ili kusaidia marejesho. Hii ni fursa kwa kila
mtanzania kuweza kujiunga na kupatiwa mkopo.
#UJUMBE: "Nipo
studio na Banana Zorro tunatengeneza wimbo kwa ajili ya matangazo ya
Vicoba na video itatengenezwa hapo kesho, siku ya jumatatu itakua hewani
katika media mbali mbali"