Saturday, May 17, 2014
ADAM KUAMBIANA AFARIKI DUNIA
Muigizaji na Muongozaji wa filamu za Bongo Movie Adam Philip Kuambiana amefariki dunia ghafla leo asubuhi kutokana na Maumivu ya Tumbo yaliyoanza asubuhi ya leo wakati akiwa anashoot movie yake na kina Q Chillah, Adam Kuambiana alilalamika kuwa tumbo linamuuma na kuwaomba wenzake wamuwahishe hospitali na kabla ya kufika njiani akapoteza maisha, mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya taifa Muhimbili, na kwa wakati huu waigizaji, wadau mbalimbali na wana familia wako maeneo ya Leaders Club kwa ajili ya kujadili msiba wa Adam Kuaambiana.
Comments System
facebook