"Hi Dayna, sikufichi ulikua unahusika/
au mtoto wa uswazi ' akijichubua ' haimaanishi anaukimbia uafrika?/
nisikize Dayna..please.. najua uko busy kiaina na hizi ni aina tu za uchizi au kama vipi bye DAYNA/
HUUH.. now back to you fools/
Akizungumzia ishu hii Fid Q amedai kuwa katika ngoma hiyo hamzungumzii Dayna Msanii bali anamzungumzia Dayna msichana anayeishi nae kitaani maeneo ya Mikocheni kwa Nyerere, Dayna huyo wa kiafrika alikua mweusi sasa hivi amejichubua ngozi yake na kuwa mweupe, Fid Q alienda mbali zaidi na kuchambua kitaalam kuwa wadada wanaofanya hivyo wanaua melanie kitu muhimu sana kwenye ngozi ambacho hupatikana zaidi kwenye ngozi nyeusi ya kiafrika chembechembe ambazo huilinda ngozi isiunguzwe na jua.
Kwa Upande wa Dayna Msanii, yeye nilikutana nae Ijumaa iliyopita pale Club Billicanas nikamdokeza kuhusu line ya Fid Q akanijibu kuwa hajawahi kuiskia wala kuambiwa so akaniahidi atai download ngoma hiyo aisikilize vizuri, Leo nilipomvutia wire Dayna akanijibu ameisikia na anamuheshimu Fid Q kwa wazo lake ila kwa wakati huu amepunguza kidogo kutumia mikorogo