Monday, June 23, 2014

PICHA: NDOA YA AMINI NA FARIDA WA KANTANGAZE


Msanii wa bongo flava kutoka Tanzania House of Talent Amini Mwinyimkuu jumapili iliyopita  tarehe 22 mwezi wa sita 2014 alifunga ndoa na msanii mwenzake wa bongo flava anayefahamika kwa jina la farida aliyeimba wimbo wa "kantangaze", ilikua ni mida ya saa mbili usiku msikiti wa banzi magomeni Kagera, Amini alifika na wapambe wake wasiozidi kumi ndani magari kama matatu, bwana harusi alikua ndani ya Prado iliyokua ikiendeshwa na Ally Choki na Best Man wake alikua Dancer Maarufu "Super Nyamwela" hakukua na msanii wa bongo flava hata mmoja, ndoa ilifungwa majira ya saa tatu kasoro usiku baada ya swala ya ishaa, baada ya hapo Amini akaenda kuchukua jiko lake mtaa wa pili kutoka msikitini ambapo ni nyumbani kwa baba yake mkubwa Farida, kufika pale ndugu wa bibi harusi nao walikua wachache kama 20 hivi, kwa hiyo hakukua na shangwe saaaana, vigelegele kwa mbaaali, watu wakapiga msosi Aumini akaonyeshwa wife wake kisha picha zikapigwa baada ya hapo kama saa nne kasoro usiku Tafrija ikaisha na Amini akamchukua Mke wake na kusepa.

Kutoka Kushoto ni Baba Mkwe akiwa ameshikana mkono na  Amini, katikati ni Ustadh Akifungisha ndoa ndani ya Msikiti
Amini na Baba Mkwe wake baada ya Ndoa kufungwa


Amini na washkaji zake wakipiga msosi nyumbani kwa kina Farida
Kushoto ni Ally Choki na Kulia ni Super Nyamwela, wasanii pekee waliofika kwenye Harusi.


Bi Harusi Farida akiwa hajapaka Hina tofauti na Maharusi wengi wa kiislam wanavyofanya kwenye ndoa zao.
Kulia ni Dada wa Bi Harusi
Ndugu wa Bi Harusi

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.