Said Ally Mrisho alielezea mkasa mzima kupitia mahojiano aliyofanya na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM ambapo watu mbalimbali wameweza kumchangia fedha na vitu vya kumsaidia kuendesha maisha yake,hasa kumuingizia kipato kwani kwa sasa hawezi tena kufanya shughuli zake za kila siku baada ya kutobolewa macho na mtu anaefahamika kama 'Scopion' mapema mwezi uliopita eneo la Buguruni Jijini Dar es salaam.
Miongoni mwa misaada aliyopoke ni pamoja na TZS milioni 10 ambazo amepewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salam,Paul Makonda aliedai kuwa yupo kwa ajili ya kusaidia wanyonge na wenye mahitaji kama alivyoagizwa na Rais Magufuli huku akiahidi kumlipia gharama za elimu ya wasioona ili aweze kuwasiliana kwa njia ya alama ikiwa ni pamoja na kumnunulia fimbo maalumu ya kumsaidia kutembelea.
Mbali na Mkuu wa Mkoa,Said amepewa msaada wa pikipiki 5 ambapo kati ya hizo,2 ni msaada kutoka kampuni ya Infotech na 3 zikiwa ni msaada kutoka TSN.Pia ndugu Admjee amemsaidia Said Bajaji 2 ambapo vyote hivi vimepatikana kutokana na juhudi za RC,Makonda kutafuta watu wa kumsaidia bwana Said.
Kwa upande mwingine GSM kupitia ushawishi wa Mkuu wa Mkoa imesema kuwa itamnunulia Said nyumba ya kuishi ambapo baada ya kushukuru alilizwa angependa nyumba hiyo inunuliwe maeneo gani na Said alipendekeza nyumba hiyo iwepo eneo la Tabata,Dar es salam kwani ndilo eneo alilolizoea kutokana na kuishi hapo tangu mwaka 1999.
Kwa upande mwigine Mwanamuziki Diamond Platnumz amejitolea msaada wa TZS milioni 2 hii ikiwa ni baada ya Said kwenye mahojiano yake kudai kuwa moja ya vitu alivyo-miss kuvitazama ni pamoja na video ya wimbo 'Salome' wa Diamond Pltnumz,hali iliyomlazimu Mwanamuziki huyo kufika Clouds fm kutoa msaada huo.
Said Ally amabae ni baba wa familia ya watoto 5,kabla ya kukubwa na mkasa huo wa kutobolewa macho na mtuhumiwa "Scopion",alikua akifanya ya kinyozi maeneo ya Tabata.
Mtuhumiwa 'Scopion',anaedaiwa kumtoboa macho Said anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi na tayari amefikishwa mahakamani na kusomewa mashataka yanayomkabili ili haki iweze kupatikana.