Mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja kiongozi
mwanzilishi wa bendi maarufu Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni ya kule
Ujerumani,juzi kati Kamanda Ras Makunja aliwekwa kiti moto au kigoda
cha moto na kituo cha TV cha Offener Channel ya Ujerumani. mwengozaji wa
kipindi katika mahojiano hayo Bw.Fischer alimkutanisha Kamanda Ras
Makunja na wataalam na wadau wa muziki wa kimataifa.
Akikaribishwa
katika kipindi hicho mwanamuziki Ras Makunja ametajwa kuwa jamii ya
ujerumani inauthamini na kuukubali mchango mchango wake wa kutumia
muziki katika
kutokomeza ubaguzi,historia imemtaja Kamanda Ras
Makunja na kikosi kazi Ngoma Africa band kuwa kuanzia mwaka 1993
alikubali kuzunguka ujerumani nzima kufanya maonyesho ya "WE ARE ONE"
onyesho liliofanikiwa kuwaunganisha wageni na wenyeji
kazi ambayo haikuwa rahisi lakini ilifanikiwa.
Lakini
pia wadau wa muziki na mtangazaji walitaka kujua inakuaje ? kwa muda wa
miaka 21 Ngoma Africa band inadumu na kuendelea kuwanasa washabiki kwa
wingi ??
Kamanda Ras Makunja akijibu swali hilo
japokuwa alionekana si wakutaka kuweka hadharani kila mbinu,lakini
alifunguka kwa kusema kuwa muziki unachezeka lakini pamoja na kuchezeka
pia wanamuziki wa bendi ya Ngoma Africa band ni watumishi wa washabiki
na wadau wa muziki kwa maana hii bendi inamilikiwa na washabiki na wadau
ambao wao ndio wanayoitangaza. Sisi tuna vyombo vya muziki tu.Mimi
naongoza bendi tu lakini wamiliki ni washabiki na wapenzi wa Ngoma
Africa band , bandi hii ni sauti ya umma wa kimataifa pia ni sauti ya
wasio sikika "Voice of speachless" ambayo inasikika kimataifa Ras
Makunja alisema.
RAS MAKUNJA ALIPOITUMIA FURSA KWA KUWAOMBA MAPOROMOTA KUWAPA NAFASI WASANII WA TANZANIA !! walio nyumbani
Kama
kawaida yake Kamanda Ras Makunja bila kujisihau wapi anatoka yaani
mtanzania aliyekunywa maji ya bendera! alipoulizwa juu ya vipaji vya
wafrika?
Kamanda Ras Makunja moja kwa moja aliwaomba wadau na maporomota wa kimataifa
kuwapa
nafasi kubwa wanasanii waliopo nyumbani Tanzania kuja kushiriki
maonyesho ya kimataifa, Ras Makunja aliwaomba na kuwashawishi maporomota
na wadau hao
kuwa nchi ya Tanzania ina utajiri wa maelfu ya
wasanii wenye vipaji vya ajabu wakiwemo wanamuziki,watengenezaji wasanaa
za mikono wanawake kwa wanaume,wacheza maigizo,sarakasi,wachoraji, nendeni
Tanzania mkaonane nao ,wapeni nafasi wasanii hawa muone jinsi watakavyo
kuja kufanya sanaa ambazo hapa ulaya ni adimu sana .
Ninawaombeni
nendeni Tanzania na mkitaka msaada wangu wa kuwaelekeza mimi nipo
Tayari - Kamanda Ras Makunja alimalizia kwa kuwaomba wadau na
maporomota.
Kamanda huyu wa Ngoma Africa Band Ras Makunja alionekana kutumia fulsa kwa
kuwapigania wasanii wa nyumbani ili wapate nafasi zaidi ya kimataifa.
Nje
ya uringo alipoulizwa mbona ameifagilia Tanzania sana na swali lilikuwa
wasanii wa Afrika, Makunja alijibu kwa mkato heti hata Umoja wa mataifa
kila nchi ina balozi wake na akatimua zake.
burudika nao at www.ngoma-africa.com
wape shavu at www.facebook.com/ ngomaafricaband