Monday, October 13, 2014

NAY WA MITEGO NA BIASHARA YA VIFAA VYA SHULE

Nay wa Mitego
Rapper Nay wa Mitego sasa hivi yupo katika mchakato wa kuzalisha Madaftari pamoja na Counter Books kwa ajili ya matumizi ya shule za chekechea mpaka vyuo vikuu, Nay amesema tayari ameshapata tenda kwenye baadhi ya shule zinazopatikana mkoa wa Mara hivyo mwezi wa kumi na mbili anatakiwa awe amewasambazia na pia yupo kwenye mchakato wa kuomba tena kwenye shule za jijini Mbeya, Nilipomuuliza kwanini amewekeza kwenye biashara ya vifaa vya Shule Nay wa Mitego alinijibu hii inatokana na Nature ya Bishara yenyewe Madaftari hayaozi kwa urahisi labda ya yaliwe na mchwa na yamwagikiwe na maji hivyo ana uhakika akiweka pesa yake kwenye biashara hii haiwezi kumwangusha, lakini pia anataka ku inspire wanafunzi wasome kwani elimu ndio ufunguo wa maisha, Nay akamalizia kwa kwa kuwasisitiza wasanii wenzake wa bongo flava na wa mbalimbali maarufu watumie muda wao vizuri kwani umaarufu ukiyumba kuna kuwa na sehemu ya kuegemea.
Add caption

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.