Monday, January 26, 2015

IDRIS SULTAN ASEMA ALISTAHILI KUMILIKI JUMBA LA KIFAHARI ILI KULINDA HADHI YAKE

Toka atangazwe kuwa mshindi wa shindano la BBA mwishoni mwa 2014 kila mtu alitamani kuona Idris atafanya nini cha kwanza kwenye dola laki tatu alizojishindia.

Sasa taarifa ikufikie kwamba Idris Sultan amenunua mjengo wake ikiwa ni moja ya malengo yake, yani ni moja ya vitu ambavyo angevisogeza kwenye maisha yake.
Stori yake ilianzia 21 January pale alipopost picha ya nyumba ya gorofa na kuandika neno moja tu; "Guess........". 
Ambapo baadhi ya mashabiki walianza kumpongeza kwa kujipatia mjengo wake.  

Kwa manyumba ya kifahari kama hii ya Idris Tazama Extreme Vacation Homes Tuesday, 27 January saa 21:30 CAT katika Travel Chanel.
Alhamisi, 22 Januari usiku Idris alipost tena picha ya nyumba yake na kulalisha kwamba ni nyumba yake huku akimshukuru Mungu kwa kumpatia nyumba mpya kwa kuandika; "Thank you for my new house."

Nyumba ina sebule mbili, ipo Dar es Salaam na Idris alikua anatarajiwa kuanza kuishi rasmi kwenye nyumba hiyo hii Januari tarehe 25.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.