Tamasha lililofanyika Jumamosi iliyopita pande za Leaders limezua utata baada ya vituko vingi kutokea huku staa wa Bongo Fleva,Ali Kiba kuhusishwa na imani za kishirikina baada ya kushindwa kupita getini na kuruka ukuta.
Mlinzi wa getini hapo amezungumza na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa Ali Kiba alifika getini lakini cha kushangaza hakupita mlangoni aliruka ukuta na kuingia ndani.
‘’Ali Kiba alifika hapa wenzake mimi nilikuwa hapa getini lakini nikashangaa ameruka ukuta’,alisema mlinzi huyo.
Ali Kiba akizungumzia tukio hilo alisema halikuwa tukio la kishirikina ila alishindwa kupita getini kwa sababu watu walikuwa wengi.
Fununu hazikuishia hapo inasemekana eti Ali Kiba alishindwa kumpa mkono msanii mwenzake Mwana Fa huku baunsa wake akimzuia msanii huyo kumsalimia Ali Kiba, Akijibu kuhusu hili Kiba amesema kweli tukio la baunsa kumzuia Mwana Fa lilitokea kweli lakini kwa wakati huo alikua ametazama ukutani na lipokuja kugeuka na kushtukia ishu hiyo walisalimiana vizuri na Mwana Fa.
Katika tamasha hilo baadhi ya mashabiki walifanya vurugu kwa kurusha chupa za maji wakati wasanii hao walivyokuwa jukwaani.
Ali amejibu kuwa ule ni ushabiki.

Sikiliza You Heard ilivyokua kwenye XXL