Chifu mmoja kutoka kaunti ya Baringo nchini Kenya amejikuta katika mazingira magumu baada ya kukutwa na chakula cha wizi kilichotolewa na Serikali ya Kenya kama msaada.
“Ameshikwa kwa sababu alibomoa stoo ya chakula na kuchukua chakula kashikwa akiwa na mafuta ya three little ya kupikia chakula”– Mwananchi.
Licha ya Chifu huyo kuwa na funguo ya ghala hilo aliamua kuvunja mlango wa ghala hilo kwa lengo la kuficha ushahidi, lakini Polisi waliokuwa doria wakamkuta akiwa amebeba vitu mbalimbali na kumkamata.
”Mwizi yote ni mwizi… wengine akiiba si wanatandikwa hapa ? sasa yeye anafichwa huko kwa nini? Wananchi waone kamani ni mwizi ni mwizi tu ni kama nyoka ndogo na kubwa yote ni sawa, sasa mtoto ya nyoka ni nyoka hata kubwa akiuma mtu anakuwa mgonjwa, sasa mwisi ni mkubwa lasima mwisi mkubwa aonekane”– alisema mwananchi mmoja aliyeonekana kukasirishwa na kitendo hicho.
Wakazi wa eneo hilo wamesema tabia ya wizi wa chakula cha msaada umekithiri sana huku wakilalamika kuwa hata kidogo kinachopatikana watu hupeana kwa kujuana huku walioathirika kwa njaa wakikosa, wengine hula mizizi,
Chifu huyo alipelekwa kituo cha Polisi kwa ajili ya kupelekwa Mahakamani.
Unaweza kuisikiliza na kuangalia story yote hapa kwa kubonyeza play.