Monday, February 9, 2015
HAKIMU AAGIZA SUGE KNIGHT AENDE JELA
Katika kusikilizwa kesi ya mauaji inayomkabili repa Suge Knight jana Februari 9, Jaji aliagiza repa huyo apelekwe jela kwanza mpaka kesi itakavyokuwa imeitwa tena mwezi Machi. Mwanasheria wa suge Knight na mwendesha mashtaka waliomba muda zaidi kuandaa na kupitia vizuri dhamana iliyosikilizwa pia.
Kiongozi huyo wa zamani wa Death Row alishtakiwa kwa mauaji kwa kugonga mtu na gari na kumuua hapo na kuondoka, mtu huyo aliyegongwa anaitwa Terry Carter na alimjeruhi mtu mwingine anayeitwa Cle “Bone” Sloane mwezi uliopita huko Compton.
Kesi ya Suge Knight atarudi mahakamani Machi 20, katika kufuatilia sakata hili endelea kutembelea gazeti la makorokocho kujua mwisho wa kesi hii Suge Knight atashinda au atashindwa kesi hii.
Comments System
facebook