Tuesday, February 10, 2015

IMERIPOTIWA NICKI MINAJ NA DRAKE WANATAKA KUTOKUWA NA UPANDE KATIKA MZOZO UNAOENDELEA KATI YA WAYNE NA BABY



Wakati Lil Wayne alipotangazia ulimwengu anataka kuondoka lebo yake ya siku toka akiwa mdogo ya Cash Money Records, haraka watu wakaanza kujiuliza itakuwaje kwa wakali Nick Minaj na Drake.

Mambo yalizidi kuwa mabaya zaidi baada ya Lil Wayne kufungua kesi ya madai ya dola milioni 51 kutoka lebo hiyo. Na wikiendi iliyoisha mwanzilishi wa Cash Money Bryana “Birdman” Williams a.k.a Baby alizuiliwa kuingia kwenye pre-party ya grammy awards ya Nick Minaj kitu kilichoanzisha uvumi kwamba repa huyo mkali wa ngoma ya “feeling myself” alimzuia Baby asiingie ili kutunza heshima na kuwa mwaminifu kwa Wayne.

TMZ iliongea na chanzo ambacho kipo karibu na Minaj kinasema hiyo haikuwa ishu sana, kutokana na chanzo kutoka kwa Birdman ni kwamba Baby alinyimwa kuingia katika club ya usiku ya 10AK kwa sababu club ilikuwa imepangwa kufungwa ndani ya dakika 15. Pia Minaj alikuwa tayari ameshaondoka kwenye club hiyo wakati  Baby alipowasili.

Watu wa ndani pia wamesema kwamba wote Nicki na Drake walionekana kutokuwa na upande wowote katika kesi hiyo inayomusisha Wayne na Cash Money. Wayne anataka alipwe mauzo ya mara mbili ya platinum yaw echini yake kama angeachana na Cash Money.

Drizzy na Minaj wanategemea na kutumaini mambo yatakuwa sawa bila kuvunjika kwa YMCMB.

Mwezi Desemba Nicki aliongelea ugomvi huo na alisema anajua Wayne na Baby wanapendana na watamaliza yote yanayotakiwa kupatiwa suluhisho, alisema yeye ni Young Money na atakuwa na Wayne popote lakini Baby ameafanya kazi kubwa katika akili yake kuwa imara.

Uongozi wa Wayne wanae Nicki kama mteja, mwanzilishi wa The Blueprint Group Cortz Bryant tayari wazi anampa support Wayne kutengana na CMB.

 “Wayne aliibeba Cash Money nyuma yake kwa miaka 10 ambapo hakuweza kuondoka na alifanya hili kwa maamuzi yake, Mtu mkweli ninayemjua duniani, hastahili kupitia ujinga unaoendelea kwa sasa katika game” aliandika Bryant katika instgram account yake.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.