Paul Walker aliacha dunia na
Hollywood katika mshituko kufuati kifo cha ghafla, muigizaji huyo star wa
movies ya Fast & Furious alifariki Novemba 2013. Paul Walker alifariki
akiwa na umri wa miaka 40 akiwa baba wa mtoto mmoja, alikufa kwa ajali mbali
mbaya ya gari akiwa anaendeshwa na rafiki yake Roger Rodas wakiwa na gari aina
ya 2005 Porsche Carrera GT. Gari iligonga nguzo ya taa na kuwaka motoa Paul
Walker alifariki hapo hapo.
Ryan Dunn baada kuweka maisha yake matatani baada ya kufanya
utani mmbaya kupitia TV, star huyo mwenye vituko Ryan Dunn alikufa kwa ajali ya
gari baada ya Porsche 911 ilipotoka nje ya barabara huko Pennsylvania 2011.
Taarifa za polisi ziliripoti kwamba star huyo aliyekuwa na
miaka 34 alikuwa amezidisha mara pindi kiasi cha pombe kinachoruhusiwa kisheria
alikuwa akiendesha speed ya 130 mph ndipo gari ikapata ajali na kuwaka moto,
Wote Ryan Dunn na abiria Zachary Hartwell aliyekuwa kwenye gari walikufa .
James Dean kama
ungekutwa ndani ya gari yake aina ya Porsche Spyder 550 huwezi toka ilikuwa
ajali mbaya, aligongana na gari nyingine ambayo ilikuwa ikikatiza mbele yake,alikufa
baada ya kuvunjika shingo, James Dean alifariki akiwa na miaka 24 tu ilikuwa
Septemba 1955.
Maisha ya Princess Diana yalikatizwa Agosti 1997
pale gari aliyokuwa akiendesha iligonga nguzo za pembeni za barabara za chini
huko Paris. Princess Diana majeraha aliyokuwa ameyapata akafariki baadae
hospitali, sio Diana wala aliyeongozana nae, Bwana Dodi Fayed alikuwa amefunga
mkanda wakati wakipata ajali hiyo. Wakati huo huo dereva aliyeitwa Henry paul
ambae paia alikufa alikutwa na kiasi kikubwa cha pombe katika mwili wake.
Grace Kelly miaka 15 kabla ya kifo cha Princess
Diana, Princess Grace wa Monaco alihusika katika ajali mbaya ya gari Septemba
1982. Muigizaji huyo wa Hollywood alipata stroke wakati akiendesha gari yake
aina ya Rover, gari ikaanguka ina kubiringita mita 120 chini ya bonde, Grace
aliyekuwa na miaka 52 alikufa kutokana na majeraha siku iliyofuata . Princess
Stephanie ambae nae alikuwa ndni ya gari
alipona.
Lisa “Left eye” Lopez ajali mbaya iliyotokea huko
Honduras ilikatiza maisha ya mwanamuziki kutoka kundi la TLC Aprili mwaka 2002.
Left Eye alifariki akiwa na umri wa miaka 30, alikuwa katika kipindi cha
mapumziko. Lopez alikuwa akiendesha gari akagonga miti miwili na gari kupinduka
baada ya kulikwepa gari lingine alilokuwa agongane nalo.
Jayne Mansfield Law & Order: Star Mariska
Hargitay alikuwa na bahati kuokoka kutoka katika ajali mwaka 1967 ajali
iliyomchukua mama yake Jayne. Mansfield alikuwa ni abiria akiwa katika kiti cha
mbele wakiwa na gari aina ya Buick Elecktra 225 ya mwaka 1966, waligonga tela
ya trekta kwa nyuma huko Louisiana. Hargitary ambae alikuwa na umri wa miaka
mitatu tu alikuwa amekaa nyuma na ndugu zake wawili ambao wote walipona.
Marc Bolan muimbaji wa rock wa Uingreza, alifariki
Septemba 1977 baada ya gari yake aina ya Mini 127GT ambayo mchumba wake Gloria
Jones alikuwa akiendesha iliingia kwenye ukingo huko kusini mahgaribi mwa
London. Bolan ambae alikuwa na umri wa miaka alikufa papo hapo, taarifa
zilieleza kwamba Bolan hakujifunza kuendesha gari kwa sababu hakupenda kufa
mapema.
Dottie West muimbaji wa muziki wa Country,alikuwa
amechelewa katika party ya Grand Ole Opry, ndipo gari aliyokuwa ndani yake
ikapata ajali wakati akielekea eneo la tukio. Jirani yake ambae alikuwa
akiendesha gari alishindwa kuicontrol gari ikapinduka. Dottie alipata majeraha
ya ndani ikiwa ni pamoja na maini, alikufa siku chache mbele Septemba 4, 1991.
Randy “Macho
Man” Savage, ulimwengu wa mieleka ulipoteza star wake Mei 2011, alifariki kwa
mshtuko wa moyo akiwa kwenye gari yake. Taarifa za Florida Highway Patrol,
Savage alikuwa na umri wa miaka 58, akiwa kwenye Old Jeep Wrangler iligonga
mti, mke wake Lynn ambae alikuwa kwenye gari alipona lakini Savage alifariki
kutokana na majeraha.
Sam Kinison, ni mchekeshaji maarufu, alikuwa na umri wa
miaka 38 wakati alipofariki baada ya gari aina ya pick-up truck kupata ajali na
gari hiyo aliyokuwa akiendesha. Muhubiri huyo wa zamani ambae alifariki wakati
akiendesha akitokea nyumbani kwake California kuelekea kwenye show yake ambayo
tiketi zilikuwa zimeuzwa na kuisha (sold out) huko Laughlin Nevada, alipata
tatizo linalojulikana kama dislocated neck na majeraha mengine. Ni kijana
mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwepo ndani ya agri hilo katika viti vya nyuma
alikuwa akinywa pombe.