Wednesday, February 11, 2015

UNAJUA TAREHE VIATU VYA KANYE WEST, YEEZY 750 BOOST ADIDAS VITAKAYOINGIA SOKONI?




 Viatu hivyo (sneakers) vitawafikia watu siku ya Jumamosi, Februari 14, ikiwa kwa mara ya kwanza itakuwa ni New York, viatu hivyo vilivyosubiriwa kwa hamu na mashabiki, sneakers hizi zitatoka na watu wataweza kupata pairs zao.

 Juzi Februari 9, Adidas walituma meseji kupitia Confrimed sneaker app, ikisema kwamba Yeezy 750 Boost zitatoka wakati wa NBA All Star weekend, baadae siku hiyo ikawa rasmi kwamba zitatoka Februari 14.

Siku adidas waliyotangaza ni sawa na ile ripoti iliyotoka mapema kwamba Yeezy Boost zitatoka wakati wa New York Fashion Week, ambayo itakuwa Februari 12 – 19, lakini rasmi itakuwa Jumamosi 14 Februari 2015.


Wikiendi iliyoisha mshikaji wa karibu na Wes,t Ibn Jasper alivujisha picha za sneakers hizo kupitia instagram, toka viatu hivyo vilivyoonekana kwenye miguu ya Yeezy, Pia Big Sean alivaa  wakati wa performance yake kwenye L.A House of Blues na Puffy Daddy alimshukuru Ye kumpatia mzigo.

Sneakers hizo zitatoka Jumamosi Februari 14, kwa mara ya kwanza New York, mashabiki wataweza kupata Yeezy Boosts kupitia adidas, Champs, na Foot Locker store kwa kutumia App iliyothibitishwa ya adidas. (adidas’s Confirmed app).

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.