Unapozungumzia gemu la muziki aina ya hip hop hususani kwa
wakina dada, huwezi kuacha kumtaja mkongwe Miss Eliot, watu wengi hasa
mashabiki wake walikuwa wakimuombea siku moja arudi studio na kufanya ngoma,
mara ya mwisho alifanya show wakati wa Superbowl 49, hilo liliwapa tumaini
mashabiki kwamba kuanzia pale angerudi studio na kupiga kazi.
Miss Eliot amepost kupitia ukurasa wake wa twitter
akionekana n mtayarishaji aliyekuwa akifanya nae kazi kwa karibu mkali
Timbaland, kwenye picha wameonekana wako bize studio.