Tuesday, April 28, 2015

BASATA: MSANII ATAKAYEJITOA KWENYE TUZO SERIKALI KUMFUNGIA KUFANYA MUZIKI NCHINI


Baraza la Sanaa la Taifa kupitia kwa mratibu wa Tuzo za KTMA ndugu Kwirijira maregesi amezungumzia vitendo vya baadhi ya wasanii kujitoa kwenye tuzo hizo na kushutumu waandaaji wa Tuzo hizi ambao ni serikali kupitia baraza la sanaa Taifa (Basata) akitolea mfano tukio la hivi karibuni pale Kiongozi ya bendi ya Fm Academia "Nyoshi El Sadat" alipoongea na vyombo vya habari na kuishutumu Basata eti kuna upendeleo kwenye mchakato wa Utoaji wa tuzo, sasa basata wamesema kuwa Wamemtaka Msanii huyo kuthibitisha madai yake kwa maandishi na vielelezo vingine.
Nilipomuuliza Je kwa wasanii watakaojitoa kwenye Tuzo hizi, ndugu Maregesi amesema wanatakiwa kuliandikia Baraza barua ya kujitoa lakini sambamba na kujitoa wajue kwamba moja kwa moja watakua hawana kibali cha kufanya muziki nchini.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.