Licha ya kusuburiwa kwa muda mrefu na polisi kwenye nyumba yake usiku wa kuamkia August 31 huko Las Angeles na hatimae kukamatwa na polsi ikiwa ni baada ya mwanamke aliedai kuwa Mwanamuziki Chris Brown alimtishia na silaha nzito,hatimae Mwanamuziki huyo ameachiwa kwa dhamana ya $250,000.Hata hivyo ni bahati mbaya kwa Chris Brown kwani licha ya kuwa historia ya makosa ya jinai,polisi wamedai kuwa wakati wa upekuzi kwenye nyumba yake walikuta begi lenye madawa ya kulevya na silaha.
Chris Brown,aliekaa chini mwenye kofia nyekundu.
Mara baada ya kupata Dhamana hiyo Mwanasheria wa msanii huyo Mark Geragos amedai kuwa mteja wake yupo salama na kudai kuwa tuhuma za Baylee Curran mwanamke anaedai kuwa Breezy alimtishia na silaha barabarani kama ilivyoripotiwa na mtandao wa
TMZ hazina ukweli wowote kwani Mwanamke huyo ana historia ya kuhusihwa na matukio ya fujo ambapo inadaiwa kuwa mnamo mwaka 2013 Mwanamke huyo akiwa na marafiki zake au kibongo tuseme na mashosti zake kwenye mgaahawa wa Pizza aliwatoroka wenzake akiwa na mkoba aina ya Louis Vuitton huku mkoba huo ukiwa na kiasi cha $200,Kadi za benki na nyaraka nyingine hivyo licha ya madai yake dhidi Brezy, Polisi wamedai kuwa Mwanamke huyo alikua akisakwa na
maafisa wa NYPD.
Byleen Curran.
Chris Brron ataendelea kupunga upepo uraiani akisubiri kuripoti tena Mahakamani tarehe ishirini ya mwezi September.
Kama kawa Team Makarokocho tutanyapia kitakachojiri na kuwa-uptodate.
Chris Brown.