Msanii anayeunda kundi la Navy kenzo Aika Marealle maarufu kama AIKA anafikiria kurudi tena shule ili kuongeza elimu zaidi,Msanii huyo ambaye kwa sasa ana degree ya biashara ambayo alisomea India alisema hayo mara baada ya kupewa nafasi ya kutoa speech fupi kwa wanafunzi wa sekondari ya mwendakulima iliyopo kahama mkoani Shinyanga walipofanya ziara na wasanii wengine ilikuweka msisitizo kwenye elimu kabla ya show ya fiesta iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Uwanja Wa Taifa wa kahama.
"Mimi ni msanii na nimesoma masomo ya biashara, nina degree lakini pia nitasoma zaidi kupata Masters hadi PhD. Sanaa ni biashara na kusoma kunakuongezea maarifa, naomba muwaheshimu walimu wenu na wazazi wenu" alisema AIKA
Pia anawakumbusha mashabiki na wapenzi wa muziki mzuri kuwapigia kura Navy kenzo kwernye tuzo za African Youth Choice Award kwa kubonyeza Hapa.