Wednesday, August 31, 2016

Licha ya kusitishwa kwa maandamano ya Ukuta,matukio ya Spt.mosi 2016 hayatasahaulika.



Hatimae Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kusitisha maandamano na mikutano yake chini ya operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta nchini (Ukuta),kwa muda wa mwezi mmoja.
                       Mh.Freeman Mbowe,M/KT-CHADEMA.

 Katika taarifa yake kwa wanahabari jijini Dar  es salam Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amedai kuwa kamati kuu ya chama hicho kwa kuzingatia ushauri wa viongozi wa dini wamefikia uamuzi huo ili kuwapa nafasi viongozi hao wa dini kutafuta suluhu ya mzozo wao na seriikali ya Rais John Pombe Magufuli....“CHADEMA tunaomba kuwatangazia watu wote kwamba tunaahirisha mikutano ya kisiasa na maandamano yote kwa muda wa mwezi mmoja,” alisema Freeman Mbowe.

 Hata hivyo taarifa za kunyapia nyapia zinadai kuwa baada ya kuvuja kwa  tetesi kuwa Chama hicho kikuu cha upinzani kimeahirisha maandamano hayo,Jeshi la Polisi limewataka viongozi wa chama hicho waliokamatwa juzi kutokwenda kuripoti polisi kama walivyoagizwa na jeshi hilo.
Taarifa ya kutotakiwa kuripoti polisi mnamo Spt.-mosi kama iliyotakiwa awali, zimethibitishwa na Mh.Mbowe mwenyekiti wa chama hicho Taifa na Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro   ambae alitakiwa kuripoti makao  makuu ya polisi  ikiwa ni pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ambae alikua mgombea uraisi kwa mwamvuli wa vyama UKAWA,Katibu Mkuu, Vicenti Mashinji na Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika.

Hata hvyo hatua ya kuwakamata viongozi wa chama hicho mnamo August 29 na jeshi la polisi ni muendelezo wa jeshi hilo kupiga marufuku mikutano ya kisiasa kuanzia ile ya ndani na nnje ambapo jeshi hilo liliwakamata viongozi hao wandamizi wa chama hicho wakati wakiendelea na kikao chao cha Kamati Kuu (CC) kwenye Hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam.

Taarifa zilieleza kwamba, katika kamatakamata hiyo, mtafaruku mkubwa ulizuka baada ya viongozi wa jeshi hilo kutaka Chadema kusitisha kikao chake cha CC (Kamati Kuu), kilichokuwa kikiendelea hoteli hapo na kupelekea viongozi waandamizi wa chama hicho kutakiwa kwenda kutoa maelezo  yao makao makuu ya  polisi na kutakiwa kiripoti tena September mosi siku waliyopanga kufanya maandamano.


Mara baada ya taarifa za kusitishwa kwa maandamano hayo ya UKUTA,Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salam Simon Sirro,ametoa kauli ya kupongeza uamuzi huo.....“Nawashukuru sana viongozi hawa kwa uzalendo waliouonesha kwa kusimamisha mikutano na maandamano yao..,” amesema Siro.

SEPMTEMBER MOSI -2016  ILIVYOKUSANYA MATUKIO.

1.Chama kikuu cha upinzani CHADEMA kilipanga,kufanyika maandamano na mikutano isiyo na kikomo nchi nzima chini ya operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta (Ukuta).

 2.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anakua kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kuhamia rasmi mjini Dodoma ikiwa ni kutimizwa kwa ahadi ya serikali ya Raisi John Pombe Magufuli kuhamia kwenye mji huo uliopo katikati ya nchi.
 3.Jeshi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),linaadhimisha miaka 52 tangu kuanzishwa kwake kufanya shughuli za usafi na kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali ya nchi.
 4.Kupatwa kwa jua,tukio ambalo kitaalam linafahamika kama  Annular Eclipse ambalo,hutokea pale jua na mwezi zinapokuwa kwenye mstari mmoja ambapo umbo la mwezi linaonekana kuwa dogo zaidi kuliko umbo la jua.
Wanayansi wanasema kwamba September 1, 2016 Tanzania ndio itakuwa sehemu pekee ambayo kupatwa huko kwa jua kutaonekana vyema na kuwavutia watalii wengi.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya Uingereza imeripoti kwamba kupatwa huko kwa jua kutaanza kwenye bahari ya Altantic, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Msumbiji, kisiwa cha Madagascar kisha kwenye Bahari ya Hindi.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.