Thursday, September 1, 2016

Dj Khalid ku-host tuzo za Hip Hop za BET 2016.





Dj Khalid ameendelea kubaki kwenye headline za burudani kwani licha ya kushiriki kwenye music tour ya Beyonce inayofahamika kama "Formation World Tour",huku album yake ya "Major Key" yenye hits zilizowajumuisha mastaa wengi wa muziki Marekani ikifika namba moja kwenye chart za Billboard Hot 100,hatimae Khalid ambae ni balozi wa heshima wa mtandao wa snapchart amepata dili jingine la kuwa Host wa tuzo maarufu za muziki zinazofahamika kama BET HIPHOP MUSIC zinazotarajiwa kufanyika jumamosi ya September 17 mwaka kwenye ukumbi unaofahamika kama "Cobb Energy Performing Arts Centre" jijini Atlanta na kuoneshwa rasmi kwenye vituo vya televisheni October 4 mwaka huu.
 Licha ya kuwa host wa Tuzo hizo zinazoandaliwa na kituo maarufu cha BET (Black Entertaiment Tv),Dj Khalid ametajwa kuwania tuzo hizo kwenye vipengele tisa ikiwemo ‘DJ of the Year,’ ‘Best Hip-Hop Video,’ ‘MVP of the Year,’ ‘Track of the Year,’ ‘Album of the Year,’ ‘Hustler of the Year,’ ‘People’s Champ Award’ na vipengele pacha vya ‘Best Collabo Group’.
                                                  Jay Z na Dj Khalid

“I am extremely honored to be a part of such an incredible show that has watched me grow as an artist and mogul throughout my career,” ...... “The Hip Hop Awards are synonymous with a night of stellar performances and tributes to the greatest hip hop artists of our time. I am excited to bring cloth talk and the major keys to the Hip Hop Awards for an iconic and memorable show!”.Alisema Dj Khalid kupitia taarifa yake kwa wanahabari.






Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.