Friday, September 2, 2016

Rihanna ajichora tattoo maalum kwa ajili ya Drake.



 Mahaba niue...!! Ndo tunavyoweza kusema kwani licha ya wawili hawa kuficha mahusiano yao kwa muda ni wazi kuwa Mwanamuziki Rihanna yupo mapenzini na rapper mzaliwa wa Toronto,Canada Drizy Drake baada ya Rihhana kuamua kuchora tattoo maalum akionesha mapenzi yake kwa rapper huyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa mtandao wa  TMZ tattoo hiyo ilichorwa August 31,2016 mara baada ya wawili hao kupigana mabusu jukwaani  waki-perfom.

Tattoo hiyo yenye picha ya Samaki -Papa inadaiwa kuwa ujumbe wa mapenzi kwa Drake ambae taarifa za kunyapia nyapia kutoka kwa watu wao wa karibu zinadai kuwa Rihhana ameamua kuchora mchoro huo baada ya Drizy kumzawadia RiRi mdoli mwenye umbo la samaki huyo mapema kabla ya kufanyika kwa tuzo za MTV Video Music Awards 2016 ambapo  wakati rapper huyo akimkabidhi Rihanna tuzo ya heshima inayofahamika kama "Michel Jackson Vunuard Award" alielezea hisia zake juu ya Rihanna na kudai kuwa alianza kuhisi mapenzi kwa mrembo huyo tangu akiwa na miaka 22 huku wakitazamana kimahaba na kuukumbatiana.



Hata hivyo mahusiano ya wawili hawa yanaonekana kuwa na mafanikio kwani kupitia colabohits walizoshirikishana kama  "Whats My Name","Take Care" na "Work" zinazopatikana kwenye album zao tofauti.
 Nauona mdoli uleeeeeee....kwenye mkobaa....!! #UbuyuMtamuWaShilawadu    


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.