Friday, September 2, 2016
Tahadhari kwa watumiaji wa mtandao wa Whatsapp.
Mtandao wa WhatsApp umekuja na maboresho mapya ambapo sasa wateja wa mtandao huo wataweza kuruhusu taarifa zao kutoka katika App hiyo na kutumika kwenye akaunti zao za mtandao wa Facebook.
Imeeelezwa kuwa Facebook wanataka taarifa za watumiaji wa mtandao wa WhatsApp ili kuwarahisishia wao kazi ya kuwaunganisha watu na mambo ya kibiashara.Baadhi ya taarifa ambazo zitatumwa kwenye mitambo ya Facebook pindi utakapoiruhusu WhatsApp yako, ni pamoja na namba ya simu za watumiaji wa huduma ya WhatsApp ili kuboresha mfumo wa marafiki wa Facebook (Friends Recommendations) na pia mfumo wa matangazo.
Watu wengi hawajafurahishwa na maboresho haya na wengi kuamua kuizuia WhatsApp isitume taarifa zao kwenye mtandao wa Facebook.
Kama unataka kuizuia WhatsApp kutuma taarifa zako, fuata hatua hizi.
Comments System
facebook