Friday, September 2, 2016

Rais Magufuli ziarani Zanzibar,mkutano wa CUF wapigwa Stop.

      Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa kwenye majukumu yao ya ulinzi na usalama.

Chama cha wananchi CUF mapema leo kimezuiwa na jeshi la polisi kufanya mkutano wao  na waandishi wa habari ili kupisha ziara ya raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania,John Pombe Magufuli iliyoanza mapema  leo.
 Rais Magufuli na Mkewe Mkewe Mama Janeth Magufuli wakilakiwa na wakazi visiwani humo mara baada ya kuwasili  kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shekhani Mohamed amedai kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na eneo ambalo CUF walipanga kufanya mkutano kuwa karibu na uwanja atakaoutumia Rais Magufuli kuwahutubia wananchi.

Kwa upande wake katibu wa CUF Wilaya ya Chakechake,Salehe Nassor Juma ameelaani  na kushangazwa na maamuzi ya jeshi jeshi la polisi visiwani humo kwa madai kuwa lengo halikua kufanya mkutano wa hadhara bali mkutano na waandishi wa habari na kudai kuwa walikamilisha taratibu zote za mkutano wao ikiwemo kutoa taarifa kwenye idara ya Habari Maelezo na kupewa kibali.

Hata hivyo Katibu huyo wa CUF ameongeza kuwa dhumuni la mkutano wao lilikua ni kuunga mkono uamuzi wa baraza kuu la chama hicho kumsimamisha uanachama aliekua Mwenyekiti wa chama hicho Prf.Ibrahim Lipumba pamoja na viongozi wengine 10.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.