Thursday, September 1, 2016

Wanawake waandamana vifua wazi nchini Marekani.

  Wakati hapa nchini mikutano ya kisiasa na maandamano ikipigwa kufuli na jeshi la polisi kwa sababu za kiusalama,mamia ya Wanawake nchini Marekani wameandamana kwenye mitaa ya jiji la Los Angeles wakiwa vifua wazi ikiwa ni maadhimisho ya sikukuu inayofahamika kama "Woman's Equality Day",ikiwa ni kumbukumbu ya kusheherekea siku taifa hilo kubwa duniani kutoa uhuru kwa wanawake kupiga kura.




Makundi ya wanawake waliandamana wakizunguka fukwe za "Oceanside na Venice,Los Angeles huku tukio hilo likawavuta mamia ya watu waliojumuika kwa kwa kupiga picha huku baadhi ya  wageni wakinekana kushangazwa na maandamano hayo yaliyokua yakipewa ulinzi wa polisi.


Sio Los Angeles tu bali pia makundi mengine ya wanawake yaliandamana kwenye mitaa ya Broadway,New York City ambapo maandamano hayo yalihitimishwa na sherehe maalumu kwenye miji ya New Hamphire na Denver.


Sasa  vuta picha kibongobongo ishu kama hii ingekuwepo unadhani ingekuwaje......kama wakiwa wamevaa nguo tu tunakulaga...wakitembea uchu jeee...tunatafunaga..mie simooo #UbuyuMtamuWaShilawadu. Doh.



Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.