Monday, October 24, 2016

"Kuna mpango wa kuniua" .Seif Sharif Hamad adai.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF),Seif Sharif Hamad jumamosi ya tarehe 22,Oktoba 2016 alikata keki kwenye sherehe ya mika 73 ya kuzaliwa kwake mbele ya ndugu wa familia na wanachama wa chama hicho kwenye sherehe iliyofanyika kwenye ofisi za chama hicho Vuga,mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa CUF,Seif Sharif Hamad akikata keki kwenye hfla hiyo,kulia ni Naibu katibu Mkuu waa chama hicho Zanzibar,Nassor Ahmed Marzui.


Hata hivyo sherehe hiyo ilimalizika kwa taharuki baada ya SEIF ambae ni Makamu mstaafu wa serikali ya mseto ya mapinduzi ya Zanzibar kuwaambia wageni waliohudhuria sherehe hiyo kuwa,kuna mpango umeendaliwa wa kumkamata na kumpeleka Dar es Salaam kwenda kuhojiwa na kisha kuwekewa sumu ili kutoa uhai wake ila Mungu amekua akimlinda na kuhoji kuwa kama amekua kitoa kauli za uchochezi kwanini atolewe uhai wake badala ya kufikishwa mahakamni.

Hata hivyo Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais serikali ya Zanzibar,Mohamed Abood alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo alidai kuwa serikali itazijibu  kisheria huku akimtaka mwandishi wetu kuwasiliana na Jeshi la Polisi juu ya madai ya SEIF.

Kamanda wa Jeshi  la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo alijibu kuwa hana taarifa juu ya madai ya SEIF na kuongeza kuwa taarifa hizo anazisikia kwa mwandishi wetu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa uchuguzi wa makosa ya jinai nchini,Salum Msangi amemweleza mwandishi wetu kuwa wanafanya uchunguzi ili kuthibitisha kama kweli tuhuma hizo zimetolewa na SEIF.

"Bado tunafanya uchunguzi,tunataka kuthibitisha kama ni kweli kuwa yeye ndie alietoa tuhuma hizo".Alisema Msangi.

Chanzo:thecitizen.co.tz.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.