Monday, October 24, 2016

Jay Z kutumbuiza kwenye kampeni za Hillary Clinton siku moja kabla ya uchaguzi.



Rapper na mmiliki wa lebo ya muziki ya Rock Nation,Jay Z atatumbuiza kwenye tamasha la kampeni za mgombea urais wa Marekani kwa chama cha Democratic,Bi.Hillary Clinton siku moja kbla ya uchaguzi huko Cleveland,Ohio.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi iliyothibitishwa kutoka kwa rapper huyo ila kwa mujibu wa mtandao wa  Cleveland.com,  mtu wa karibu kutoka kwenye kambi ya kampeni za Bi.Clinton amethibitisha 'Jigger' kutumbuiza kwenye tamasha hilo kwenye jimbo la Ohio linalotajwa kuwa upinzani mkubwa likiwa na lengo la kuwahamasisha raia kupiga kura.

Hii haitakua mara ya kwanza kwa Jay Z kushiriki kwenye kampeni za kisiasa kwani miaka miine nyuma aliungana na Bruce Springsteen   kwenye tamasha la kampeni za Rais Barack Obama huko Columbus siku moja kabla ya uchaguzi ambapo kwenye tamasha hilo alinukuu moja ya mashairi yaliyopo kwenye wimbo wake maaarufu wa "99 Problems" na kuwaambia watazamaji "I got 99 problems and Mitt ain't one",Ikumbukwe kwamba katika uchaguzi huo  Rais Obama alikua akichuana na Mitt Romney wa Chama cha Republican.

 Jay Z,Bruce Springsteen na Rais Obama kwenye kampeni za chama cha Democratic,2012.

Taarifa hizi zimekuja wakati ambao mgombea wa chama cha Republican,Donald Trump akiwa kwenye vita ya maneno na mastaa wengi wa muziki nchini humo hasa wanamuziki wa 'Hip Hop' akiwemo rapper YG,Napsey Hussle,Macklemore,Rick Ross na T.I,Huku Bi.Clinton akipata sapoti ya rappers kama Pusha T,Common,Chance The Rapper na Will.i.am.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.