Friday, October 14, 2016

VIDEO :Tazama mapokezi ya heshima aliyopata Mwl.Nyerere nchini Marekani July 15,1963.(Nyerere Day Anniversary).



 Ni miaka 17 sasa imepita tangu Baba wa Taifa,Mwl.Julius Kambarage Nyerere afariki.Hivyo basi kila inapofika tarehe 14 ya mwezi Oktoba Tanzania huwa inaadhimisha moja ya siku yenye kumbukumbu kwenye taifa letu,'Nyerere Day' ikiwa ni kumbukumbu ya tarehe aliyofariki Mwal.Nyerere kwenye Hospitali ya St.Thomas nchini Uingereza.

Mwalimu alizaliwa tarehe 13 April mwaka 1922 huko Butiama,mkoani Mara na kufariki tarehe 14,Oktoba 1999.Aliingia ofisini kama Rais wa Tanzania mwaka 1964 na kuondoka ofisini mwaka 1985.

Leo tunakukumbusha ziara aliyofanya Mwal.Nyerere kama Rais wa Tanganyika nchini Marekani,na kupokelewa na Rais wa Taifa hilo kwa wakati huo,John Fitzgerald Kenedy ambae alikua rafiki mkubwa wa Mwalimu.Kwa kuthibitisha hilo ukiatazama video hii utaona ni kwa kiasi gani Rais Kenedy alimpa mapokezi ya heshima Mwalimu ambae kwa wakati huo alikua kiongozi wa taifa changa ambalo ndo kwanza lina miaka miwili tangu lipate uhuru wake.



Mwal.Nyerere alifanya ziara hiyo July 15,1963 ila kwa bahati mbaya miezi miezi minne badae Rais Kenedy aliuawa kwa kupigwa risasi.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.