Thursday, September 1, 2016

VIDEO:Stan Bakora alivyowaigiza Ney wa mitego na BASATA.




                                               Mchekeshaji,Stan Bakora.

Kama umekua ukifatilia muziki wa Bongofleva,utakua umewahi kusikia msuguano kati ya Baraza la sanaa nchini (BASATA) na msanii Ney Wa Mitego ambapo Baraza hilo limewahi kuzifungia nyimbo mbili za msanii huyo ikiwemo "Shika adabu yako" na " Pale kati patamu" ambapo kutokana na Ney kupuuzia maelekezo ya baraza hilo,ilimlazimu kulipa faini ya kiasi cha milioni moja kama adhabu kutokana na maudhui ya nyimbo za msanii huyo kwenda kinyume na maadili.
                                                       Ney wa mitego.

Sasa basi...Mchekeshaji Stan Bakora ameamua kutumia mgogoro huo kama sehemu ya sanaa yake kwa kuigiza kama Ney huku mchekeshaji nguli,Pembe akiigiza kama Afisa wa Baraza hilo.Haijafahamika kama Pembe ameigiza nafasi ya Charles Mngereza ambae ni Katibu wa BASATA ila kimaudhui tunaweza kusema ipo hivyo.

JIONEE UTUNDU WAO HAPA.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.