Thursday, November 17, 2016
"Simba imefanya biashara kichaa kumsani Okwi",Mchambuzi abainisha.
"Miezi 18 iliyopita simba ilimuuza Okwi kwa ada $110,000 kwenda timu ya Sonderjyske ya nchini Dernmark"..."huko kapigishwa benchi kwa kukosa kiwango ila cha ajabu sasa hivi simba wanamuhitaji kwa $120,000 hii ikimaanisha kuwa Simba SC itamuongezea $20,000 zaidi huku kiwango chake kikiwa kimezidi kushuka zaidi"..."Hajacheza mechi kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi sita hadi kakosa nafasi katika timu yake ya taifa,Simba ni maharage ya wapi kumchukua huyu tena anachukuliwa bila kocha kuonekana anamhitaji au laaa"..."KUMRUDISHA OKWI SIMBA NI USHABIKI SIO UCHEZAJI WAKE".
Hayo ni maoni ya Shaffih Dauda,mchambuzi wa soka nchini na mtangazaji wa habari za michezo mara baada ya uongozi wa wekundu wa msimbazi kudaiwa kumrudisha kikosini mshambuliaji wake wa zamani raia wa Uganda,Emmanuel Okwi.
Comments System
facebook
