Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

Thursday, January 5, 2017

Riyad Mahrez Mchezaji Bora Wa Afrika Mwaka 2016



Kiungo wa Leicester city Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka.
Mahrez mwenye miaka 25 raia wa Algeria aliyeisaidia Leicester kushinda taji la ligi kuu soka England msimu uliopita, tiyari ameshinda tuzo ya mcehzaji bora wa England sambamba na mchezaji bora wa BBC Afrika.

Mshambuliaji wa Senegal na klabu ya Liverpool Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang walikuwa wakiwania tuzo hiyo pia.
Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.
Denis Onyango wa uganda na klabu ya Memelodi Sundowns akishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani.
Mchezaji bora kwa kina dada imeenda kwa Asisat Oshoala wa Liverpool na timu ya taifa ya Nigeria huku timu bora ya mwaka ikiwa ni Uganda.

Thursday, December 22, 2016

Mourinho Na Mpango Wake Juu Ya Man United.

Kocha wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa anataka kusalia katika kalbu hiyo kwa muda mrefu zaidi kwa kuwa anapenda maisha yake na timu hioyo.
Mourinho mwenye umri wa miaka 53, alijiunga na klabu hiyo mwezi Julai, na sasa wako katika nafasi ya sita katika jedwali la ligi baada ya mechi 17.
Mnamo mwezo Oktoba, raia huyo wa Ureno alisema kuwa hoteli anayoishi ni janga wakati ambapo kikosi cha United kilikuwa kikiweka matokeo yasioridhisha.
Najua kwamba ipo siku moja wataleta mkataba mpya, nitatia saini.
Mourinho ameongezea kwamba hatoelekea kufunza nchini China ,ijapokuwa amekiri kwamba fedha za China zinavutia kila mtu.
Kiungo wa kati wa Chelsea Oscar amehusishwa na uhamisho wa Shanghai SIPG, ambapo huenda akalipwa kitita cha pauni 400,000 kwa wiki.
Nataka kusalia katika timu yenye changamoto kubwa ya kujipatia ushindi

Saturday, December 17, 2016

Obi Mikel kubwaga manyanga Chealsea.

Kiungo wa Chealsea John Obi Mikel yupo mbioni kusitisha huduma ya kuitumikia klabu ya Chelsea kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari,akidaiwa kuwa kwenye mipango ya kwenda kucheza ligi kuu ya China ambapo zaidi ya klabu mbili zimeonesha kumtaka Mikel mwenye umri wa miaka 29.

Kiungo huyo raia wa Nigeria hajaonekana kwenye mchezo wowote msimu huu tangu kuwasili kwa kocha Antonio Conte ambae ameshindwa kumpa nafasi kwenye mfumo wake wa 3-4-3.

Taarifa imekuja wakati ambao Chelsea imetengeneza kiasi cha  £52m. baada ya kumuuza kiungo wao Oscer kwenye klabu ya China inayofahamika kama Shangai SIPG.

Kiungo huyo alijiunga na The Blues mwaka 2006,akiwa amecheza michezo 374,akishinda mataji mawawili ya Ligi ya Uingereza,manne ya Kombe la FA na mawili ya Kombe la klabu Bingwa Ulaya.



 

Thursday, November 17, 2016

Rooney awaomba radhi mashabiki baada ya picha zake akiwa 'amezima' kuvuja.



Nahodha huyo alihudhuria sherehe hiyo ya harusi katika hoteli ambayo timu ya taifa ya Uingereza ilifikia wakati wakicheza mechi ya kimataifa.


Amesema ingawa picha hizo zilipigwa wakati wa kujipumzisha, "hazifai kwa mtu wa hadhi yake" hivyo kuwaomba radhi mashabiki wa soka nchini humo hii ikiwa ni baada ya gazeti la The Sun la Uingereza kuchapisha picha hizo ambazo zinamuonesha Rooney, 31, akiwa amelewa kwenye sherehe usiku wa Jumamosi baada ya mechi ya England ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Scotland.

Hata hivyo Rooney hakucheza mechi ambayo Uingereza walitoka sare 2-2 na Uhispania Jumanne kutokana na kusumbuliwa na jeraha la goti.

"Simba imefanya biashara kichaa kumsani Okwi",Mchambuzi abainisha.


"Miezi 18 iliyopita simba ilimuuza Okwi kwa ada $110,000 kwenda timu ya Sonderjyske ya nchini Dernmark"..."huko kapigishwa benchi kwa kukosa kiwango ila cha ajabu sasa hivi simba wanamuhitaji kwa $120,000 hii ikimaanisha kuwa Simba SC itamuongezea $20,000 zaidi huku kiwango chake kikiwa kimezidi kushuka zaidi"..."Hajacheza mechi kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi sita hadi kakosa nafasi katika timu yake ya taifa,Simba ni maharage ya wapi kumchukua huyu tena anachukuliwa bila kocha kuonekana anamhitaji au laaa"..."KUMRUDISHA OKWI SIMBA NI USHABIKI SIO UCHEZAJI WAKE".


Hayo ni maoni ya Shaffih Dauda,mchambuzi wa soka nchini na mtangazaji wa habari za michezo mara baada ya uongozi wa wekundu wa msimbazi kudaiwa kumrudisha kikosini mshambuliaji wake wa zamani raia wa Uganda,Emmanuel Okwi.

Wednesday, November 9, 2016

Lukaku kuhama Everton..!

Mshambuliajj huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na Klabu hiyo kwa mkopo mwaka 2013 kabla ya kujiunga rasmi na klabu hiyo kwa kitita kilichovunja rekodi cha pauni milioni 28 mwezi Julai 2014.



Licha ya kuwasilisha ombi la kuhama msimu uliopita ,Romelu Lukaku amefunga mabao saba kati ya 15 yaliofungwa na Everton katika ligi msimu huu.




''Iwapo Romelu angeendelea kucheza Everton hadi mwisho wa wakati wake najua angeacha kitu nyuma''......''Uwezo wake ni mkubwa na juu zaidi ya Everton'' anasema Kocha wake,Ronald Koeman.


Hata hivyo Everton imesema kuwa iko tayari kumpatia Lukaku kandarasi ya muda mrefu na kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu hiyo.

-BBC.

Thursday, October 13, 2016

PICHA:Watoto 2 wa Zalatan Ibrahimovic wajiunga na timu ya watoto ya Man-United baada ya timu hiyo kumsaini mtoto wa Wayne Rooney mwenye umri wa miaka 6.


Wakati sakata la Mshabuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza kuhusu kiwango chake na ushiriki wake kwenye timu ya taifa  likiendelea kutokota,Klabu ya Manchester United imemjumuisha mtoto mkubwa wa Mshambuliaji huyo  kwenye 'Academy' ya timu ya watoto ya klabu hiyo ambapo amekua akifanya mazoezi na timu ya watoto ya klabu hiyo.

Mtoto wa Wayne Rooney,Kai.


Kai Wayne Rooney mwenye umri wa miaka sita ataungana na watoto wa Mshambuliaji mwingine wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic ambae nae amewapeleka watoto wake wawili,Max (10) na Vincent (8) ambapo pia watajumika na watoto wa wakongwe wengine kama Michel Carrick,Ryn Giggs na Nick Butt ambao nao watoto wao wamejumuishwa kwenye timu hiyo ya watoto ya klabu hiyo.

Wayne Rooney na watoto wake,kwenye moja ya michezo ya Manchester United.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun,klabu hiyo imepanga kukuza vipaji vya watoto wa mastaa hao walioitumikia klabu hiyo kama sehemu ya kuenzi mchango wao na sifa waliyoipatia klabu hiyo.

  "The hope at the club is some of their dad’s talent has rubbed off on the youngsters"..."Manchester United is  known for its  youth development, and this is just another stride towards finding stars of the future,United have some of the best youth coaches in the world, and the players know they’re in the right place".Sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.

Tuesday, October 11, 2016

PICHA:Real Madrid kutumia 'euro' milioni 400,kubadili muonekano wa uwanja wa Santiago Bernabeu.


Klabu ya soka ya Real Madrid imepanga kufanya ukaratabati kwenye uwanja wake maarufu Santiago Bernabeu uliopo jijini Madrid,ukarabati unaotarajiwa kubadili muonekano wa juu wa uwanja huo,Rais wa Klabu hiyo tajari Ulimwenguni Florentino Perez amesema ukarabati huwa utagharibu kiasi cha 'euro' milioni 400.
Uwanja wa Santiago Bernabeu utakavyokua baada ya ukarabati.

Hata hivyo kwa upande wa watazamaji hawatazidi 81,000 ila kutakuwepo na siti mpya 3,000 zitakazofidiwa siti zitakazotolewa.

"We will see a dramatic transformation of the Santiago Bernabeu," ......"This stadium is one of the emblematic icons of our city and we want to make it one of the best stadiums in the world and the undisputed symbol of the strength of our capital." .  Perez alisema.


Ukarabati huo utakaoanza mwaka ujao,unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Rais wa Klabu soka ya Real  Madrid, Florentino Perez (kushoto),akiwa na Meya wa Jiji la Madrid Manuaela Carmena.

Baada ya kukuri kutumia 'Cocain',Bondia Tyson Fury kupokonywa ubigwa wa WBO.


Bingwa wa uzani wa juu wa ndondi duniani, Mwingereza Tyson Fury amepewa siku 10 na  Shirikisho la ngumi za kulipwa Ulimwenguni WBO, kueleza ni kwa nini asipokonywe  mkanda wake wa ubingwa.



Bondia huyo mwenye umri wa miaka 28 Alijiondoa kwenye pambano  la marudiano na Wladimir Klitschko wa Ukraine mapema mwezi huu kwa sababu ya matatizo ya kiakili huku akikabiliwa na   mashtaka ya kutumia dawa zisizoruhusiwa,hii ikiwa ni baada ya kukiri kutumia madawa ya kulevya 'coccain' ili kukabiliana na msongo wa mawazo kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga wiki iliyopita.

 Tyson Fury (kulia) kwenye pambano lake na Wladmir Klitschko.

Mwenyekiti wa WBO Luis Batista-Salas amesema Fury huenda akapoteza mkanda huo kwa kutoshiriki mapigano, kuvunja mkataba na kwa kutumia dawa zilizoharamishwa kwenye michezo.

Hata hivyo amesema WBO wanajali sana hali yake ya kiafya na wanamtakia afueni ya haraka.
Bondia huyo hajapigana,tangu amshinde Klitschko Novemba mwaka jana.

Monday, October 10, 2016

Uchunguzi wa kifo cha mchezaji aliefariki baada ya kupigwa na mpira shingoni kuanza rasmi Australia.

Uchunguzi rasmi juu ya kifo cha mcheza Kriketi Philip Hughes unatarajiwa kuanza rasmi nchini Australia.


Mchezaji huyo alifariki miaka miwili iliyopita baada ya kupigwa na mpira shingoni wakati wa mchezo huoJijini Sydney ambapo jeraha alilopata lilisababisha ubongo wake  kuchanganyika na damu na kumsabishia kifo siku mbili baadae.


Wachunguzi watachunguza kama kulikua na uwezekano wa kutumia kifaa kingine cha kuuokoa maisha ya mchezaji huo kwani mapema mwaka huu tathmini huru ilionesha kuwa kutumia kofia ngumu na ya kisasa ingeweza kuzuia ajali hiyo iliyopelekea kifo cha mchezaji huyo.
-BBC.

Zidane kutupiwa virago Real Madrid.

KOCHA wa timu ya Real Madrid, Zinedine Zidane, amekiri kuwa anafahamu ipo siku atatupiwa virago kama hatafikia malengo ya klabu hiyo aliyowahi kuitumikia kama mchezaji.



Kauli hiyo ya Zidane inatokana na mustakabali wa maisha ya kocha huyo kuwa matatani hasa baada ya timu hiyo kupata matokeo ya sare katika michezo minne mfululizo ambapo nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa aliiongoza Madrid kutwaa taji lao la 11 Ligi ya Mabingwa msimu uliopita akiwa kocha wa timu hiyo kwa mara ya kwanza huku akisisitiza kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa haogopi kutupiwa virago kama kocha wa klabu hiyo tajiri duniani.

“Nafurahia vilivyo kile nikifanyacho. Nina fursa ya kipekee. Naipenda kazi yangu ambayo si rahisi mara zote, lakini nataka kujifunza kuwa bora zaidi"...“Najifunza kila siku kufanya kazi na wachezaji bora. Nina kikosi cha kipekee, iwe tunashinda au kushindwa bado ni wachezaji wema,”.Alisema Zidane.

Madrid hawajawahi kutoa sare mechi nne mfululizo kwa kipindi cha miaka 10 kabla ya msimu huu kutokea.
Hata hivyo, kocha wa zamani wa timu hiyo, Fabio Capello, hivi karibuni alieleza kuwa mwelekeo mbaya wa timu hiyo unasababishwa na nyota wake, Cristiano Ronaldo ambaye hayupo katika hali nzuri kimwili.
Capello alitoa kauli hiyo na kuongeza kuwa tangu msimu uanze nyota huyo hayupo katika kiwango kizuri baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu katika michuano ya Euro 2016 ambayo Ureno ilifanikiwa kuwa mabingwa wa michuano hiyo.

Friday, October 7, 2016

VIDEO:Bondia afariki dunia baada ya kushuka ulingoni.

Bondia Mike Towell (25),raia wa Scotland amefariki dunia baada ya kupoteza pambano lake na Bondia Dale Evans kwenye round ya tano pambano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa St Andrews Sporting Club Septemba 29,2016.

 Mike Towell,(kulia).

Baada ya kupoteza pambano hilo hali yake ilibadilika na kukimbizwa hospitali ambako baadaye alifariki dunia ambapo ripoti ya Madaktari imeonesha kifo cha Mike kilisababishwa na kuvuja kwa damu nyingi kwenye ubongo baada ya fuvu lake kupata madhara kutookana ngumi nzito alizopigwa maeneo ya kichwani.



    Mike akiwa na wapambe wake.

Kabla ya kupoteza pambano hilo bondia huyo aliangushwa mara mbili kwenye mzunguko wa kwanza kabla ya kuangushwa tena kwa konde zito na kushindwa kuendelea na pambano.

"absolutely heartbroken".Rafiki wa karibu wa Towell,Chloe Ross aliambia mtandao wa Sky News.

 Hata hivyo Bondia Dale Evans aliepigana na Towell, ameungana na mashabiki wa bondia mwenzake hasa wa mchezo huo nchini Scotland,Wakiendesha kampeni ya kuchangisha michango kwa ajili ya familia ya Towell.

Thursday, September 22, 2016

Picha:Kilimanjaro Queen's yapokelewa Dar.


Kilimanjaro Queens imetua Dar ikiwa na kombe la CECAFA Women’s Championship 2016 walilolitwaa nchini Uganda kwa kuifunga timu ya taifa ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets kwa magoli 2-1.


 Timu hiyo imepeta mapokezi kutoka kwa viongozi wa serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya michezo, viongozi wa TFF pamoja na mashabiki ambao walijitokeza kwenye uwanja wa ndege wa Mw. JK Nyerere.


Wednesday, September 21, 2016

Rais Magufuli aungana na Watanzania kuipongeza Kilimanjaro Queen.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza timu ya taifa ya soka la wanawake ya Tanzania bara Kilimanjaro Queens kwa kutwaa kombe la baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Women’s Championship) baada ya kuifunga Kenya goli 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliofanyika  mjini Jinja nchini Uganda.


Hii hapa taarifa ya Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Matokeo ya raundi ya 3 #EFL (Capital One).

 Usiku wa Jumanne ya wiki  hii zilichezwa mechi za raundi ya tatu ya kombe la EFL ambapo zamani lilikuwa likijulikana kama Capital One. Mechi iliyovuta hisia za mashabiki wengi wa soka ilikua kati ya mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita, Leicester City ambao walifungwa mabao 4-2 dhidi ya Chelsea.


Matokeo Raundi ya 3 #EFLCup
Everton 0-2 Norwich
Derby County 0-3 Liverpool
Nottingham Forest 0-4 Arsenal
Newcastle 2-0 Wolves
Leeds 1-0 Blackburn
Leicester 2-4 Chelsea
Bournemouth 2-3 Preston
Timu zilizoshinda zimetinga Raundi ya nne.

Monday, September 19, 2016

Baada ya Man-United kukubali kichapo,Madee ajibu post ya Pogba Instagram.

Klabu ya Manchester United  kwa mara ya tatu mfululizo katika kipindi cha juma moja imepoteza michezo yake tena ikikubali kufungwa na klabu ya Watford kwa magoli 3-1.

Watford walikuwa wa kwanza kupata goli lilifungwa na Daryl Janmaat kabla ya Marcus Rashford kusawazisha.Ila kiungo wa Watford Zuniga alifunga ikiwa imesalia dakika saba mchezo kukamilika kabla ya Deeney  alifunga penalti katika muda wa ziada baada ya Marouane Fellaini kumchezea vibaya katika eneo la hatari.

Hii ni mara ya tatu mfulilozi kwa Manchester United kupoteza,ikishindwa 2-1 na Manchester City,baadaye ikapoteza 1-0 dhidi ya klabu ya feyenoord ya Uholanzi katikati ya wiki katika kombe la bara Ulaya.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika Mshambuaji wa Manchester United,Paul Pogba ali-post ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwashukuru mashabiki wa United na kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito hali ilipelekea mashabiki wengi kuponda ujumbe wa mshambuliaji huyo aliesajiliwa kwa kiasi cha $105m.

Miongoni mwa walitupa madongo kwa mshambuliaji huyo ni Mwanamuziki wa Bongo fleva,Madee Ali  ambae ni shabiki wa Unite alie-coment kwa kuandika "U can wapi ww rudisha mapene ya watu..ww mtu gani ufungi..mbona xhaka kafunga jana".Aliandika Madee.


 Swali la kujiuliza,kwa lugha aliyotumia Madee ujumbe utakua umefika kweli...!!!.


Wednesday, September 14, 2016

Matokeo ya mechi za UEFA zilizochezwa usiku wa Sept.14.


Neymer ageukia muziki,kuachia wimbo wiki ijayo.


Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na nahodha wa timu ya taifa ya Brazil,Neymer ameamua kuweka wazi mapenzi yake na muziki na kwa kuthibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter alipost ujumbe kwa mashabiki wake ulimwenguni na kuahidi kuwa atatambulisha wimbo wake mpya wiki ijayo.

"This Wednesday I begin my music career and I’m going to release my first song on Facebook," Ulisomeka ujumbe huo uliotazamwa na watu zaidi ya milioni 20.

 Hii sio mara ya kwanza kwa Mwanasoka huyo kuonesha hisia zake kwenye muziki kwani March 4 mwaka 2015 ilisambaa video mtandaoni ikimuonesha yeye  na mwanasoka mwenzake Dani Alves wakiimba wimbo wa Mwanamuziki Nick Jams unaofahamika kama "El Perdon" hivyo uamuzi wa Mwanasoka huyu kuingia kwenye muziki unaonekana ni sehemu ya mipango yake ya siku nyingi

Sunday, September 11, 2016

Ajibu na Mavugo waendeleza ubabe wa Simba dhidi ya Mtibwa Suger.

Magoli ya Ibrahim Ajibu na Laudit Mavugo yametosha kuifanya Simba iendeleze ubabe mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kuifunga kwa mara nyingine tena kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.Magoli yote ya Simba yamefungwa katika kipindi cha pili baada ya timu hizo kutoka suluhu katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.




Dondoo kwa namba:

30 -Namba kubwa zaidi ya jezi ilivaliwa na golikipa wa Mtibwa Sugar Abdallah Makangana.

10 -Pointi ambazo Simba imefikisha baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa.

6 Pointi za Mtibwa baada ya kucheza mechi nne. Imeshinda mechi mbili na kupoteza michezo miwili.

9 Mtibwa wapo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi baada ya mchezo dhidi ya Simba.

2 Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 10 sawa na Azam FC wanaoongoza ligi.








VIDEO:Jose Mourinho awatupia lawama mastaa wake.

Kocha wa Manchester United,Jose Mourinho amewalaumu wachezaji wake  akidai  kuwa wao  ndiyo sababu ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya mahasimu wao Manchester City kwa mabao 2-1.

                                                     Jose Mourinho.

Man United walijikuta wakipotezwa kabisa na vijana hao wa Pep Guardiola kwenye dimba lao la Old Trafford, na kujikuta wakiruhusu magoli mawili yaliyofungwa na Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho.

 Baada ya mchezo huo Mourinho alisema: "Wakati mwingine wachezaji huwavunja moyo mameneja wao".Alimwambia ripota wa Sky Sports.  “Kipindi cha kwanza walikuwa vizuri zaidi yetu"....."Tulianza mchezo huku baadhi ya wachezaji wakicheza chini ya kiwango chao cha kawaida kuanzia kwenye suala la umakini mpaka kasi ya mchezo".

              Jose Mourinho (L) na Meneja wa Man-City,Pep Guardiola wakati wa mchezo.

"Unahitaji kuwa na maamuzi ya haraka namna unavyocheza na unavyofikiri"..."Mchezaji mmoja au wawili hivi walikuwa hawapo kwenye kiwango kizuri na hali hiyo imeigharimu timu".Aliongeza Kocha huyo mwenye tambo nyingi.

Mourinho aliwaanzisha Jesse Lingard na Henrikh Mkhitaryan kwenye kikosi cha kwanza lakini aliwatoa wote baada ya kipindi cha kwanza kuisha baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.