Leo Marekani imeweka historia baada Donald Trump wa chama cha Republican
kutangazwa mshindi wa kiti cha Urais, na tayari ameanza kupokea pongezi
kutoka kwa viongozi wa nchi mbalimbali ikiwemo Rais wa Tanzania, John
Pombe Magufuli.
Rais Magufuli ametoa pongezi zake kwa Rais mteule, Donald Trump kupitia ukurasa wake Twitter.
Ameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha katika uongozi wake.
Mgombea
wa Republican Donald Trump amemshinda Hillary Clinton wa Democratic
katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongezaTrump amepata kura 278 za wajumbe, Bi Clinton akiwa na 218.Trump alishinda majimbo mengi yaliyokuwa yanashindaniwa nchini humo.