MBEYA-.Gari la Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi limesababisha kifo cha mtoto aliyekua akivuka kwenye kivuko cha watembea kwa miguu eneo la Iyunga jijini humo.
Kamanda wa wa Polisi mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari amesema mtoto huyo,Recho Lutumo (15) baada ya kugongwa alipelekwa hospitali ya rufaa Mbeya ambako alikata Roho.
Wakati ajali hiyo inatokea mbunge huyo alikuwamo kwenye gari hilo lililokuwa linaendeshwa na dereva wake,Gabriel Andrew wakielekea uwanja wa ndege,ambapo katika hali ya kushangaza gari ya Polisi iliyokuwa inaelekea eneo la tukio ilipata ajali na kujeruhi askari Polisi wanne.
Chanzo:mashuhuda/SHILAWADU.