hupenda kujiita Fuad Jamal a.k.a Mzee Baba amenaswa uwanja wa ndege wa
Mwalimu Julius Nyerere wakati akisubiri Ku kwea pipa la kuelekea
uingereza Huku akijua fika kuwa Ana kesi ya kutishia kumuua mama yake
mzazi, ina maana alipoona Hukumu inakaribia machale yakamcheza Akaona bora
akimbie
Ndipo kabla hajafanikiwa kutoroka Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wakafanikiwa kumpiga pingu mbele Ya Abiria wenzake
.
Inasemekana Mzee baba akaanza Kutokwa na Machozi Kama Mtoto mdogo, .
Mpaka
wakati huu Inasemekana Mzee Baba yupo Polisi Kwa ajili ya mahojiano na
alipojaribu kuomba dhamana ilishindikana kutokana na Mtuhumiwa huyo
kumiliki Passport mbili Za kusafiria moja ikimtambulisha Kama raia wa
uingereza na nyingine ikimtambulisha Kama Raia wa Tanzania
.
Inadaiwa
kuwa chanzo cha mgogoro Kati ya mtu na mamaake ni masuala ya Nyumba
Nyumba ambapo Bi Mkubwa aliingia mkataba Na mwekezaji flan jina kapuni,
kwamba Nyumba aliyokuwa anaimiliki ivunjwe Na kujengwa Ghorofa ambalo
chini kuna frames halafu juu kuna makazi ya watu, mchongo ukafanyika
Mama akapewa baadhi ya Vyumba kwa makubaliano kwamba baada ya Miaka
kadhaa Atamiliki Ghorofa lake lote mwenyewe, basi mama akaamua
kuwakabidhi wanae Funguo moja moja, sasa inasemekana Farid akaingiwa na
tamaa na kutaka apendelewe zaidi Kwa kupewa Nyumba Zaidi ya moja ndani
ya Ghorofa Hilo, hivyo akawa anamlazimisha mama yake Kwa kutishia
kumuua kitu ambacho mama yake alikipinga, Ndipo Jamaa huyo akawa
anamtishia kumuua na hii si Mara ya kwanza Siku ya Siku Farid alimvamia
mama yake akiwa na kundi la wahuni inasemekana kuwa Walitishia kumuua
Mama Kama akienda kinyume na makubaliano Yao, Bahati Nzuri majirani na
baadhi ya Ndugu waliskia vishindo na makelele ikabidi wakaingilie Kati na
kwenda kumuokoa mama yao, mtuhumiwa na wenzake wakachoropoka ikabidi
mama akatoe ripoti Polisi ikafunguliwa kesi na kuanza kuunguruma Ndipo
Farid alipoona maji yanamfika shingoni Akaona bora atoroke nchi, Polisi
walipopata taarifa ndo wakamnasa airport na kumtia ndani