Tuesday, December 13, 2016

PICHA:Waendesha bodaboda wamvamia Mh.Lowassa Hotelini Tabora na kuamua ku....!?

Vijana wanaojihusisha na  biashara ya usafirishaji  kwa kutumia usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda, asubuhi ya leo (jumanne) wamejitokeza kwa wingi katika hoteli aliyofikia waziri mkuu huyo mstaafu na mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA.

Katika malalamiko yao vijana hao wamelalamikia ugumu wa maisha hasa mfumuko wa bei katika mkoa huo, kukosekana kwa pesa kwenye mzunguko na hali ngumu ya maisha kwa ujumla katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Vijana hao pia wamemlalamikia Mh. Lowassa kuhusu kunyang'anywa vyombo vyao vya kufanyia kazi na waajiri wao kutokana na kutofautiana itikadi za kisiasa.


 Chanzo:Mashuhuda wa SHILAWADU,Tabora.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.