Tuesday, December 13, 2016
Rapper Young Thug anavyowakoa Watoto wa mitaani na kuwasaidia watu kupambana na Umasikini
Rapper Young Thung huenda sasa ameanza kukua baada ya kuelezea harakati zake za kurudisha fadhila kwa jamii na kuwasaidia watu kupambana na umasikini ambapo mpaka sasa anawahudumia zaidi ya watoto 10 waliokua wakiishi kwenye mazingira magumu.
Kwenye mahojiano aliyofanya na jarida la PAPER, akiwa na X-Girlfriend wake Jerrika Karlae,memba huyo wa lebo ya 'Cash Money' amedai kuwa anatataka kuwasaidia watoto wa mitaani na kukumbushia simulizi yake ya mtaani wakati alipokua na kati ya miaka 14/15 ambapo alikua akipora watu mitaani kutokana hali ngumu ya maisha.
"I never want my kids to feel like they don't have anything. I had my first child at 14/15, so you can only imagine [what it was like in the beginning]...When you're poor you do anything to survive. You rob and take...Whenever I go back to my side of town — Cleveland Ave [in South Atlanta] — I know I have to bring money, because there will be friends or cousins or people I knew from 6th grade who are going to ask me for money. My fiancée always says I look like Santa Claus, because I'm just giving everyone something".Alisema rapper huyo.
Thug ambae anatajwa kuwa chanzo cha Boss wa wake Birdman kupigana chini na Lil Wayne,kwa mwaka 2016 alifululiza kuachia Mixtape zilizokua na hits kali zilizosumbua kwenye Chati mbalimbali Ulimwenguni kiasi cha staa wa R&B Usher Raymond kuamua kumshirikisha rapper huyo kwenye wimbo wake wa "No Limit".
Comments System
facebook