Monday, June 7, 2010

Hatimaye Ndoa ya Nas na Mwanadada Kelis ya vunjwa rasmi



Ndoa ya Nas na Kelis imevunjwa rasmi na mahakama ya jijini los Angeles.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ.COM ndoa hiyo ilivunjwa rasmi siku ya Ijumaa tarehe 21 May na inavyoonekana wanandoa hao hawakutaka ishu hiyo iende public.

Pamoja na maamuzi ya mahakama lakini bado Mambo mengi hayajatatuliwa, mambo kama fidia na pesa ambazo Nas anatakiwa atoe kwa ajili malezi ya mtoto.

Mwezi wa nne Nas alimpa Kelis Dola elfu 87 ikiwa ni zaidi ya pesa alizotakiwa kulipa ambazo ni dola elfu kumi.

Watalaka hao walioana mwaka 2005 baada ya kukaa kama wachumba kwa muda wa miaka miwili.

Nas amemtuhumu Kelis kwa kumnyima kushuhudia kuzaliwa kwa mtoto wao KNIGHT julai 2009, ambae amezaliwa kipindi mchakato wa kuvunjika kwa ndoa hiyo unaendelea.

Pia alimlaumu Kelis kwa kumkataza kumuona mtoto wao wakati kesi yao ikiendelea.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.