Tuesday, June 8, 2010

Lil Kim amemdiss Bosi wake wa Zamani kwa kuingia Mkataba na Nicky Minaj


Lil Kim ameipeleka Beef yake na Nicky Minaj katika Next level kwa kumwingiza Manager wa Nicky Minaj P Diddy katika beef hiyo.



Wakati akiperform kwenye Concert mjini Baltimore, Maryland hivi karibuni Lil Kim alimdiss kwa maneno Diddy.



Kim aliendeleza vita vyake dhidi ya Nicky Minaj ndani ya Sonar Night Club ambapo alimjumuunganisha Diddy wakati akiperform wimbo wake wa Its all about Benjamin ambapo aliongezea maneno yafuatayo: Puffy anatakiwa ajionee aibu, na maneno mengine kibao ambayo hapa siwezi kuyasema, baada ya hapo Kim alimuita on stage B-More na wakaendeleza kupiga Freestyle ya kumdiss Nicky Minaj.



Nicky yuko mbioni kumalizia kusign mikataba na Diddy, wakati flani Diddy alimsifia nicky rapa mkali na ana safari ndefu kimziki na kufananisha rapa huyo na LeBron James, Tiger Woods na Kobe Bryant.



Alipofanya Interview na Kendra G, Kim alidai kuwa Nicky anatakiwa amshukuru sana yeye, aliendelea kusema kuwa madem wote wanao ingia kwenye Game tunatakiwa ku stick pamoja na nimejitahidi kuwasisitiza wote lakini wanapatwa na wivu na kunichukia wanapogundua Funs wangu wananipenda zaidi na hata siku moja hawabadiliki, anasema wanachokifanya ni upuuzi kwani yeye kama mkongwe anachohitaji kutoka kwao ni Heshima tu, anasema mambo mengi yanaendelea chini kwa chini na watu hawayajui, akaongeza kuwa huwezi kuficha ukweli, nilipokuja kupiga promo tour, ni kujikumbusha wapi tulipotoka kwasababu kama uta swagger Jack na kucopy style ya mtu basi unatakiwa kupay respect kwa muhusika.



Katika Concert nyingine iliyofanyika weekend hiyo hiyo Drake alipanda juu ya stage na kujibu Diss za Lil Kim kwa kusema maneno yafuatayo: “ Najua unawaita wanawake Malaya, lakini siwezi kusema wewe ni Malaya zaidi, siwezi kufanya hivyo kwasababu nakuheshimu, I love you too much and you look beautiful, so nataka kusema umeingia sehemu ambayo sio, sijali chochote ktakacho semwa na Lil Kim au yeyote yule, wewe ni mbaya kwasababu umeingia huku, wakati maneno hayo yanasemwa Nicky Minaj aligeuka huku anacheka na kumhugg Drake, then akamwambia Drake I Love you.

.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.