Tuesday, June 8, 2010

Sara Stokes amefungua Kesi dhidi ya T-Pain


T pain amefunguliwa kesi katika mahakama ya nchini marekani na mwandishi wa nyimbo ambae amedai T-Pain amemnyima haki zake katika wimbo walioutunga wote yaani Sara Stokes na T-pain, na walimuandikia mwimbaji mwingine wa R&B anayeitwa Jennifer Hudson

Kampuni ya Sara Stokes SARAMONY INTERTAINMENT wamefungua kesi hiyo siku ya ijumaa iliyopita katika mahakama ya MISSOURI ESTERN DISTRICT, akidai kuwa ametengeneza nyimbo na kuandika nyimbo mbili akishirikiana na T-Pain, ikiwa ni pamoja na Wimbo uliopo katika Album ya Hudson iliyoshinda Tuzo za Grammy.

Stokes anadai pamoja na Album hiyo kufikia mauzo ya Gold lakini hajapewa shavu ama Credit, kwa kuandikwa kama yeye pia ni mmoja kati ya producer na mwandishi wa Nyimbo hizo.

Stokes anadai kuwa kpindi hicho label aliyokuwa akiifanyia kazi ya OUAN ENTERTAINMENT iliingia mkataba na kampuni ya T-pain inayoitwa Nappy Boy Production kwa nia ya kuandika na kuproduce nyimbo mbili.

Nyimbo hizo zikarekodiwa katika studio ya T-pain na kwa mujibu wa madai yake yapo chini ya nyumba yaani Basement ya T-pain mjini Atlanta, Georgia.



Stokes anadai kuwa walitunga wimbo na kurekodi na T-Pain, na wimbo huo ukarushwa katika radio WHHL 104.1 ya mjini Missouri.



Stokes akashtushwa baada ya kusikia T-Pain ameingia deal na kampuni ingine kwa kumruhusu Hudson kurudia kurekodi wimbo huo bila kuweka sauti yake.

Katika madai yake ya Msingi Sara Stokes anataka aandikwe ama ijulikane Officially kwamba yeye ndio mwandishi wa wimbo unaoitwa Whats wrong na vilevile apewe mgao wake uliopatikana katika mauzo ya wimbo huo, pia arudishiwe gharama zote za kufungua kesi hiyo.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.