Tuesday, June 8, 2010

MJ avunja Ukimya Kuhusiana na Madai ya Stiggo


Hatimaye MJ ameamua kuweka kufunguka juu ya utata uliopo kati ya Label yake ya MJ Records na S&S records inayomilikiwa na Stigo Ibrahim mtanzania anayeishi jijini New york Marekani.

Stiggo Alikuwa wa kwanza kudai kuwa Label ya MJ imetumia Beat aliyoitengeneza bila ruhusa yake, na Beat yenyewe ni ya ule wimbo wa Quick Raka unaitwa Bullet, kwa muda mrefu Master jay alikaa kimya na hakujibu tuhuma hizo, lakini hivi karibuni ameamua kuvunja ukimya huo,

Master Jay amedai kuwa siku ambayo Beat hiyo inatengenezwa na MarcoChali yeye pia alikuwepo Studio na kushuhudia tangu Beat hiyo inaanza kugongwa mpaka mwisho wake, Jay akaongeza kuwa mziki hauna mwenyewe kwani chords na vifaa vya muziki ni vile vile vilivyopo siku duniani, hivyo madai ya Stiggo hayana nguvu.

Pia MJ alieleza kusikitishwa na madai hayo kwani yeye Jay wimbo wa kwanza kuurekodi wakati anaanzisha Label yake ya MJ RECORDS mwaka 1989 ulikuwa wimbo wa kundi la THE DIPLOMATS kundi ambalo ndani yake alikuwemo Stiggo, Sigon, Dola Soul na wengine, na aliwarekodia wimbo huo bila malipo.

MJ anasema hakuweza kuzungumzia ishu hiyo kwa muda mrefu kutokana na wanasheria wake kumshauri asifanye hivyo kwa wakati ule, na akaendelea kufunguka kuwa kwa sasa yeye na timu yake wanachosubiri ni Stiggo afungue madai yake mahakamani na yeye yuko tayari kupambana nae kisheria.

Msikie Master Jay hapa kama alivyoongea na 255

Cue………









Vile vile hatukuishia hapo Stiggo nae alitafutwa akasema kampuni aliyoingia nayo mkataba wa kupromote kazi zake imemshauri kutofungua kesi yoyote kwani Africa ama Tanzania Kesi za aina hiyo hazina Deal kwani gharama za kufungua kesi na wao kuja mpaka Tanzania hata wakishinda Kesi yenyewe bado itakuwa imekula kwao.

Ila Stiggo akatahadharisha kuwa iwapo Quick raka atakwenda nchini marekani na Kuperform na Beat hiyo, atajiingiza matatani na vyombo vya sheria vya marekani.

Stiggo atashuka Bongo mwezi wa Kumi na mbili mwaka huu.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.