Kushoto: AT, Mwenye Kofia nyekundu ni Muda Chriss
Muda Mfupi baada ya Habari kusambaa kama bomu la machozi kuwa Member wa Kundi la Off Side Trick (Muda Chriss) amejiengua kwenye kundi hilo na kuamua kumrudia mungu totally, Mpinzani wa Kundi Hilo kwa muda mrefu amempongeza Muda Chriss kwa kitendo hiko, na kusema kuwa mwaka 2010 wakati akihojiwa na CHANNEL 10 alitabiri hilo, na akasema kuwa Muda ni MTALII kwenye muziki wa Bongo Flava na Hana muda mrefu itabidi aachee, A.T anasema kuwa aliliona hilo baada ya kuona wazazi wa MUDA CHRISS hawataki mtoto wao afanye muziki, na MUDA kwa kipindi chote hicho ameishi huku akiwa na BEEF na wazazi wake ambao ni wacha mungu (waumini wa dini ya Kiislamu)
Alipoulizwa na Makorokocho je ni tukio gani litamfanya amkumbuke mchizi kwenye Maisha kimuziki? haya ndo maneno aliyosema:
1.... "mi nitamkumbuka kwa show ambayo tulifanya Dar Live mbagala, alinitukana sana, nafikiri yalikua ni matusi ya kuniagia, nikasema kwamba kila kitu kinapangwa na mungu."
2... "Alisema yeye ni mkali wa hizi kazi na mwaka huu atafanya kile kitu ambacho yeye anajua freshy, lakini mwisho wa siku imebidi apumzike"
3... "kule zanzibar wanasema dhulma kafara, ukimdhulumu mtu kitu chochote unakua kama umejipiga kafara."
4... "kudhulumiwa sio lazma mtu akadhulumu hela, mtu anaweza akadhulumu hata ule uwezo wa kuweza kuishi kwa amani kwa kukutafutia sababu mbaya, kwani hicho amekudhulumu haki yako ya msingi ambayo unatakiwa kuishi nayo duniani."
Mwisho wa siku AT akampongeza Muda Chriss kwa kuwa sikiliza wazazi wake na kumrudia mungu, lakini pia akasema kwamba yeye Binafsi amemsamehe Muda kiroho safy