Muigizaji wa Filamu nchini
anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth
Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake
kuhu...siana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.
Elizabeth Michael amesomewa mashtaka
hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya
Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza
vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.
Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote
Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa
kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.
Muigizaji huyo aliletwa mahakamani
hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo
alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza
kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika
gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848
BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.