Hammer Q |
Bibie Salha baada ya kuchezea kichapo |
Msanii maarufu wa muziki wa taarab Hussein Mohammed a.k.a Hammer Q jana
amempa kipigo cha mbwa mwizi mkewe Bi Salha Abdallah kwa tuhuma za
kudaiwa talaka na mkewe huyu ili aende kwa kijana ambaye yeye alikuwa
akimtamka kwa jina la Sharo baro, Mtuhumiwa huyo ambaye ndiye
anayesadikiwa kuwa chanzo cha ugomvi huo wa wanandoa hao ni Mtoto wa
Moshi william ambaye anajulikana kwa jina la Hassan Moshi.
Tukio hilo lilianzia Dar Live
ambapo kulikuwa na uzinduzi wa Bendi ya 5 star, inasadikiwa Mtoto wa
Marehemu TX Moshi William alikuwa akisalimiana na Mke wa Hammer Q na mke
wa Hammer Q akamuomba mumewe amtambulishe kwa Rafiki yake huyo (Hassan
Moshi), baada ya kumtambulisha ugomvi ndio ukaanzia hapo. Watonyaji wa
habari hiyo wakasema Hammer Q alianza kumpa kichapo mkewe huyo ambaye
alikuwa yupo kwenye maandalizi ya sherehe ya kitchen Party yake ambayo
ilikuwa ifanyike Tarehe 24/05/2013 ingawa harusi ilikuwa tayari
imeshafanyika.
Baada ya Songombingo hilo
kutulizwa na washkaji zake Hammer Q wanandoa hao wakatulia, wakashiriki
shughuli hiyo ya uzinduzi mpaka ilipoisha na baada ya hapo wakaondoka na
kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwao Magomeni ambako pia wana mji
wao ukiachilia kule kigamboni. Kwa mujibu wa Hammer Q anasema alipofika
nyumbani mkewe huyo alianza kumsemea maneno ya kashfa na kuanza kumdai
talaka na ndio hasira zikampanda na kuanza kumpelekea kipigo cha MBWA
MWIZI kwa mujibu wa majirani walioshuhudia tukio hilo, Hammer Q
aliendelea kumpiga mkewe huyo kama vile anataka kumtoa Roho, majirani
walipokuwa wanaingilia ili kuweza kusuluhisha inasadikiwa Hammer Q akawa
anasema anampiga mkewe huyo kwa sababu amemuoa na amemgaramia, tukio
hilo la kikatili lilidumu takribani nusu saa mpaka pale wasamaria wema
walipofanikiwa kumnasua mkewe huyo katika mikono ya mumewe huyo (Hammer
Q) ambaye wadau wengi wanasema ni mchezo wake kuwapa vichapo wale ambao
huwa na mahusiano nao kimapenzi kwa kisingizio cha wivu.
Hata hivyo baada ya tukio hilo
wasamaria wema walimpeleka Salha (Mke) mpaka hospitali ya magomeni kwa
matibabu na kwenda kufungua kesi katika Kituo cha polisi cha magomeni,
Wafuatiliaji wetu hawakuishia hapo ikawalazimu wampigie simu Hammer Q
kutaka kujua zaidi ana uamuzi gani kutokana na kitendo chake hicho
lakini yeye alikiri kufanya kitendo hicho cha kikatili na kuishia
kuwaomba samahani watanzania, wanafamilia ya Mkewe huyo pamoja na
majirani kwa kusema haikuwa dhamira yake ila ni POMBE tu ndio
zilimpelekea afanye kitendo kile.
Familia ya Baba yake Salha
(Mke) wametaka Hammer Q akamatwe haraka sana kwa kutenda kitendo cha
kikatili ambacho hakikubaliki kwenye jamii ya Watanzania wa karne hii,
pia kwa mujibu wa Mke (Salha) amesema Hammer Q alishamwandikia talaka
yake kwa maelezo ya talaka tatu ambayo alikata kijikaratasi kimoja na
kumwandikia kama talaka, Wadau mtatusaidia kama talaka hiyo ni halali au
La!
Taarifa zaidi tutawaletea kama
ameshakamatwa au La! ingawa majirani wanasema walipokuwa wanampigia
simu alikuwa anasema anataka kujiua kwa kudhani yeye alishakuwa amemuua
Salha (Mke) kwa sababu alipokuwa anatolewa nyumbani alikuwa amezimia hajitambui. Salha ameshonwa nyuzi kadhaa kichwani na mkononi.
wakati akihojiwa na GEAH HABIB wa leo tena ya clouds fm, Hammer Q amesema ni shetani tu alimpitia
Story kwa hisani ya
kapingaz.blogspot.com
Story kwa hisani ya
kapingaz.blogspot.com