Wednesday, April 4, 2012

KALLAGHE AKANUSHA KUMTENDA VIBAYA KEKUU

Kekuu
Director Kallaghe wa kampuni ya "Kallaghe Pictures" amekanusha Kudaiwa na Femcee "Kekuu" na hiyo ilikua ni siku tatu baada ya Msanii huyo wa Kike kudai kuwa Kallaghe anamzungusha kwa zaidi ya miezi minne na hataki kumkabidhi video, waliyokua wameshoot miezi minne iliyopita, na tayari alikua kishalipia kila kitu kama makubaliano yao yalivyokua (laki nne kwa video) Kekuu akaongeza Kuwa ameamua kwenda kwenye Vyombo vya sheria, hatua yake ya kwanza amemchukulia RB Director, na kila akijaribu kwenda kumkamata mdai wake wanamkosa, sasa Kallaghe amefunguka kuwa si kweli kama mwanadada huyo anamdai kama anavyotangaza, bali yeye Kallaghe ndio anamdai Kekuu shilingi laki moja, ndio maana akaamua kutoi edit video hiyo mpaka atakapolipwa na Kekuu, ndio atamkabidhi mzigo wake, zaidi anashanga kuskia anatafutwa na Polisi wakati yeye hana taarifa yoyote ya inayomtaka ku ripoti polisi

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.