Monday, April 2, 2012
BLACK WA USWAZI ATEMANA NA ADAM JUMA WA VISUAL LAB
Rapper black wa Uswazi hivi karibuni kupitia kipindi cha XXL ya Clouds fm ametangaza kujitoa chini ya management ya mtu mzima Adam Juma, na kwa sasa hivi yuko free hayuko chini ya mkataba wa mtu yeyote,
Alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi hiko B-twelve, juu ya sababu zilizomtoa huko, Black akajibu kuwa jamaa amekua akimweka muda mrefu bila kurelease ngoma zake kwenye radio na Tv Station, Black anasema kuwa Adam ana ngoma zake Audio zaidi ya 30 na Music Video tatu.
Black akaongeza kuwa labda jamaa (Adam) anafanya hivyo kwa sababu ana kazi yake ya kushoot video so ana mek chapaa, bila kumwangalia yeye Black atakula nini wakati kazi yake ni muziki?
Kwa kujiengua chini ya Adam Juma waliyekutana zaidi ya miaka kumi iliyopita katika Uwanja wa Baskeball wa Spider Upanga/Dar es salaam, kasha wakaanzisha Label ya “uswazi” Black anasema ameondoka na Label hiyo pamoja na wasanii waliokua wanaunda Label enzi hizo kabla ya Kujitoa chini ya Adam, na kujiunga tena hivi karibuni chini ya Uongozi wake Black, wasanii hao ni AT na Jelly wa Rhymez.
Comments System
facebook