BIBI CHEKA AWALAUMU MAJIRANI KWA KUMSINGIZIA UCHAWI
Bibi Cheka
Msanii mwenye umri mkubwa kuliko wasanii wote wa muziki wa Kizazi kipya, namzungumzia Bibi Cheka (mwenye zaidi ya miaka 50), inadaiwa huko Nyuma kabla hajawa Star, alikua akijishughulisha na Biashara ya Kupika Maandazi na Vitumbua, lakini cha Kusikitisha baadhi ya majirani zake walikua wakisambaza taarifa za Kizushi kuwa Eti Bibi Cheka ni mchawi hivyo watu wasiende kununua Maandazi kwake, ikaenda weeee akaja akabadili biashara na kuanza kufuma vitambaa, hali ikawa hivyo hivyo, lakini muda mfupi baada ya Kurecord na kurelease Ngoma Yake aliyomshirikisha Mheshimiwa Temba kwenye Audio na Video, basi heshima kidogo mtaani kwake (BUNJU) ikarudi japo bado wapo baadhi ya Haters wanaeneza taarifa hizo za kizushi, na yeye Bibi Cheka amekiri hivyo na kusema kuwa Eti sasa hivi kuna watu wanamfanyia Ushirikina, hawampendi, na kufunguka yeye Life style yake kitaani huwa anakua karibu sana na Vijana muda mwingi, Asubuhi anafuma Vitambaa vya kuuza, lakini Nje kwake kuna BAO vijana wengi wa mitaa ile ndo maskani so wanajumuika nae sana, Jioni anaenda Kwenye Uwanja wa Mpira kufanya mazoezi hiyo ndio ratiba yake tofauti na Kazi ya Music, Bibi Cheka yuko chini ya Label inaitwa "MKUBWA NA WANAWE" ya mtu mzima Saidi Fella ndani yake pia yupo DOGO ASLAY na wengine. skiza alichoongea Bibi Cheka ndani ya Segment ya YOU HEARD kwa hisani ya XXL