Dk Fauz Twaib Jaji wa mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam |
Haya haya sasa ijumaa iliyopita mahakama nchini Tanzania ilimkabidhi jaji wa mahakama kuu ya Tanzania Dk Fauz Twaib kusikiliza maombi ya uchunguzi wa umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a LULU, mambaye anakabiliwa na bo bo bo booooonge la kesi ya mauaji ya Steven Kanumba/Ze Great na maombi hayo yanatarajiwa kusikilizwa tarehe 28 Mei 2012,
Hiyo ni baada ya mawakili wanaomtete LULU wakiongozwa na Keneddy Fungamtama kuwasilisha maombi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, wakiiomba iamuru kesi hiyo isikilizwe katika mahakama ya watoto wakidai kuwa mteja wao ni mtoto.
So ikithibitika kuwa wakati kifo cha kanumba kinatokea mshtakiwa Lulu alikua na miaka chini ya kumi na nane basi adhabu itakua ndogo na ikithibitka kuwa lulu alikua na umri wa miaka 18 na kuendelea basi duh….tumwombee mungu.
Lakini Jaji aliyehusika kuchunguza umri wake, lakini ngoja nikukumbushe kesi chache ambazo Jaji Dk Fauz Twaib amewahi kuzitolea hukumu
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu kunyongwa kwa kamba hadi kufa raia wa India Vinoth Praveen kwa kosa la kumchoma visu hadi kufa Mtanzania, Abdul Basit.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Dk. Fauz Twaibu aliyesema kwamba mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Juni 21 mwaka 2011
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu, Omari Mahita, dhidi ya aliyekuwa msichana wake wa kazi anayedaiwa kuzaa naye.
Katika rufaa hiyo, Mahita alikuwa akiiomba Mahakama Kuu itengue hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ambayo ilimuamuru kupeleka gharama za matunzo ya mtoto wake Juma Omary Mahita (14) mtoto anayedaiwa kuzaa na msichana huyo Rehema Shabani.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Fauz Twaib ambapo alisema rufaa hiyo ya madai Na.149/2009 iliwasilishwa mahakamani hapo na mrufani (Mahita) anayetetewa na Charles Semgalawe dhidi ya mrufaniwa (Rehema) anatetewa Frederick Mkatambo toka Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) akipinga hukumu ya kesi ya madai Na.9/2007 iliyotolewa mwaka 2009 na Hakimu Mkazi Kihawa.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Juni 25 mwaka 2011.