MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amesema kuwa ofisi yake inakusudia kuimarisha usalama wa mkoa huo kwa kufunga kamera za CCTV zitakazosaidia kubaini matukio ya uhalifu na wahalifu kwenye mitaa ya Jiji hilo la kitalii.
Sehemu ya mitaa ya Jiji la Arusha kama inavyoonekana kupitia picha ya satelite.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa kiongozi wa ujumbe wa wabunge wa Sweden Bi. Matilda Irnkarns waliomtembelea ofisini kwake.
"Tunakusudia kuongeza usalama mkoani mwetu kwa kufunga kamera za CCTV zitakazotuonesha matukio ya uhalifu na wahalifu watakaokuwa wakiwasumbua wananchi wa Arusha, watalii na hata wawekezaji Mkoani mwetu,"......"Tunapokuwa na uhakika wa kudhibiti wahalifu tunakuwa na uhakika wa usalama na kuwavutia watalii na wawekezaji,pia wananchi wanakuwa na amani,"Gambo alisema.