Friday, September 23, 2016

"Kuhusu T.H.T. naomba msahau",Ruby afunguka.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na kituo cha Ea Radio,Ruby amesema kuwa alikuwa hana haja ya kukataa kuonekana kwenye baadhi ya nyimbo ambazo yeye ameshirikishwa ila kuna wakati mwingine watu hao walikuwa wakimzingua.

"Unajua ukisikiliza maneno ya upande mmoja unaweza kudhani labda kinachoendelea ni sawa mimi siwezi kukataa kufanya video zao sema muda mwingine unakuta wao ndiyo wanazingua, kuna muda mwingine mimi ndiyo nazinguliwa, watu wananikwamisha ili nisionekane kwenye hizo video".Aisema Ruby


Hata hivyo hit's maker huyo wa singo kama "Na Yule" na "Forever", amewataka mashabiki wake wasahau mambo yote yaliyotokea kipindi cha nyuma kati yake na uongozi uliokua ukimsimamia hapo awali na kudai kuwa kwa sasa amekuja kivingine na kuomba s support kuotoka kwa mashabiki.

Sikiliza wimbo mpya wa Ruby "Wale Wale",uliondaliwa na Mtayarishaji Man Walter.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.