Wednesday, May 29, 2013

WANAMCHAFUA ALBERT MANGWEA WAKATI AMBAO BADO MWILI WAKE HAUJAZIKWA

TANGU LINI MAREHEMU AKAZUNGUMZIWA KWA UBAYA?
Kwa taratibu za mila na desturi za makabila mengi ya Afrika, pindi kinapotokea kifo cha mwanajamii basi jamii ile nzima hukumbushana kwa kuhadithiana mazuri ya Yule marehemu wao, yako wapi hayo kwenye msiba huu wa Albert Mangwea?
Watu wanaandika na kuzungumza kwenye vyombo vya habari kuwa kifo chake kimetokana na matumizi ya kupitiliza ya madawa ya kulevya / kuji overdose.
Madawa ya kulevya si kitu kizuri kukihusisha na binadamu, kwanza ni dhambi kuyatumia kwa mujibu wa vitabu vya dini.
Je kauli kama hiyo Mama mzazi wa ALBERT MANGWEA anapoiskia, inamuumizaje? Mtoto wake je?, ndugu zake? Marafiki, na true fans? Tujiulize je wote hawa wanafurahia mnavyoropoka ropoka kwenye vi blogu, kuta za facebuk na twitter, cha kusikitisha mpaka vyombo vya habari vilivyopewa leseni navyo vinafanya kama ya facebook, je angekua ni mzazi wako au ndugu yako anazungumziwa kwa style hiyo utapenda kusikiliza au kusoma?
Tujiulize je ALBERT huko roho yake ilipo inafurahia mnayo yaropoka?
Ok Sawa tuseme ni freedom of speech/ uhuru wa kutiririka, lakini mbona Report ya Post morterm / Autopsy ambayo daktari anaitoa baada ya kuufanyia uchunguzi mwili marehemu Ngwair haijatoka?
Sasa nyinyi mmetoa wapi hayo madudu?
Katika kipindi hiki Watanzania tunataka kusikia mazuri ya marehemu wetu Albert Mangwea, pia tunataka kujua taratibu zinaendeleaje, lini mwili utarejeshwa bongo ili tumpumzishe ndugu yetu.
kwa kuandika na kusema eti amekufa kutokana na kuji overdose, mnamdhalilisha marehemu, Mnamchafua, hamkuwahi kumpenda kwa dhati bali mnakitumia kifo chake kama fursa ya kupata traffic kwenye blogs zenu, kupata watazamaji na wasikilizaji wa vyombo vyenu vya habari au kupata retweet na comments nyingi kwenye mitandao ya kijamii.
hata kama ni kweliii, sasa yanini kuyazungumza.
Watanzania tuna majonzi, acheni kutu stress katika kipindi hiki, tumewachoka.
mbona marehemu alifanya mengi mazury, tujikumbushe nayo basi.
Mungu ailaze roho ya marehem Albert Mangwea mahali pema peponi.
IMEANDIKWA NA MUHARIRI WA GAZETI LA MAKOROKOCHO www.makorokocho.blogspot.com
SOUDY BROWN.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.